Baada ya kunaswa na kamera za usalama (CCTV) zilizofungwa kwenye vyumba vya darasa, Mhadhiri mmoja (jina halikutajwa) amefukuzwa kazini na uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) tawi la Dar es Salaam kwa kubainika kufanya ngono na vitendo vingine vya ukiukwaji wa maadili -- limeandika gazeti la NIPASHE.
Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Emanuel Mjema akizungumza na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene alisema kuwa vyumba 20 vya madarasa ya chuo hicho vilifungwa kamera hizo mwezi Aprili mwaka 2013 ili kujiridhisha na taarifa za kuwepo kwa matukio ya vitendo vya ngono baina ya walimu na wanafunzi wa kike ambao walikuwa wakipewa alama za juu kwenye mitihani, wizi wa mitihani na matendo mengine yanayovunja sheria:
“Nilipoingia chuoni hapa Januari mwaka jana, nilisikia kuwa kuna baadhi ya wahadhiri wamekosa maadili, wanatoa alama za juu kwa wanafunzi wa kike kwa masharti hata kamaalifafanua Profesa Mjema.
hawajafaulu kwa kiwango hicho. Nikaona vyema tuweke vifaa hivyo ili kudhibiti vitendo hivyo,”
Alisema pia kamera hizo zimesaidia kuwadhibiti wanafunzi wenye tabia ya kuiba mitihani, kwa mfano zina uwezo wa kumvuta karibu (zoom in) mwanafunzi aliyeko darasani na kujua anachokiandika; Vile vile zina uwezo wa kutumika kutizama iwapo mhadhiri anafundishana kutoa elimu inayostahili wakati wa vipindi vya kawaida vya darasani au maelezo sahihi wakati wa mitihani.
Prof. Mjema alisema pia kuwa chuo kimeajiri walinzi kwa ajili ya kuwadhibiti wanafunzi wanaovaa mavazi yaliyo kinyume na vielelezo na maelekezo ya mavazi ya chuo hicho. Pia, walinzi hao hukagua vitambulisho vya watu wanapofika katika lango la Chuo hicho.
Naibu Waziri, Mbene, alipongeza jitihada na kuahidi kushughulikia suala la uvamizi wa eneo la chuo hicho pamoja na maombi ya kuongezewa madarasa ikiwa ni pamoja na kupewa majengo ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula cha Taifa (NFRA).