Chama cha wakulima, AFP kimemfukuza uanachama Mkurugenzi wake wa Sera na Uenezi, bwana Rashid Yussuf Mshenga kwa tuhuma za kufanya udanganyifu kuingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Wakizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa AFP Taifa, Said Soud na Naibu Katibu Mkuu, Shaib Masoud Salum wamesema mwanachama huyo ameghushi saini ya Naibu Katibu ili kujiorodhesha kwenye majina waliomba kuwa wajumbe wa bunge hilo kupitia AFP.
'Tunamfukuza Mshenga kwa sababu ametenda kosa la kugushi saini ya naibu katibu mkuu wa chama hicho ili jina lake liingizwe katika mchakato wa majina ya chama hicho'Wamesema AFP hakikupitisha jina la Mshenga kuwa miongoni mwa wajumbe wa kuteuliwa na chama kushiriki kwenye Bunge hilo. Viongozi hao wamesema mwanachama huyo ametumia njia zisizo halali kuwasilisha jina lake katika afisi ya rais Zanzibar. Aidha, chama hicho kimepanga kumfungulia
mashtaka Mchenga kwa tuhuma za kufanya udanganyifu.
KAULI YA MSHENGA
Akizungumza mara baada ya uamuzi huo kutangazwa, Mchenga amesema Mwenyekiti wa chama hicho hana uwezo wa kumfukuza uanachama isipokuwa Mkutano Mkuu wa chama hicho wa taifa, kauli ambayo ilipingwa na mwenyekiti wake, Said Soud aliyedai kuwa Msenga kwa wadhifa wake anaweza kufukuzwa uanachama na mwenyekiti na siyo Mkutano Mkuu kama anavyodai:
Cheo chake cha Mkurugenzi wa sera na mawasiliano anaweza kufukuzwa bila ya kufanyika kwa mkutano mkuu....ni nafasi nne tu za viongozi ambao kufukuzwa kwake lazima kupate baraka za mkutano mkuu.Mshenga anadai kuwa chimbuko la kuibuliwa mgogoro huo ni Mwenyekiti wake na mkewe kukosa uteuzi wa kuwa wabunge la katiba. Amesema ni choyo ya Mwenyekiti wake pamoja na kuchukizwa kukosa nafasi ya hiyo na sasa ameamua kumchafua katika jamii na kumvunjia heshima yake.
Mchenga amedai kinachofanyika kati ya Mwenyekiti wake na Naibu wa chama hicho, Shaibu Masoud Salum ni udugu wao wa kifamilia.
Mchenga ni miongoni mwa wajumbe wa vyama vya siasa upande wa Zanzibar walioteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuingia ndani ya Bunge Maalumu la Katiba kama Mjumbe.
AKIRI KUWASILISHA MAJINA YAKE NA MKEWE
Aidha, Soud alikiri kuwa ni kweli alipeleka jina lake na mkewe aliyetambuliwa kwa jina la Farida Khamis Juma na kusema hakuna kosa kwa sababu mkewe anazo sifa zote ikiwemo mwanachama halali ambaye alikuwa miongoni mwa wanawake mstari wa mbele waliokiunga mkono chama hicho.
'Kweli nilipeleka jina la Mkewe wangu katika majina ya wabunge wa bunge la Katiba lakini kwani kuna kosa gani kwa sababu anazo sifa zote ikiwemo mwanachama halali kama walivyofanya wengine'Alisema Soud.
Aidha ameilaumu Afisi ya rais Ikulu Zanzibar kwa kushindwa kufanya uchambuzi unaotokana na maelekezo ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza wenyeviti wote wa vyama vya siasa kupewa kipaumbele kuwepo katika mchakato wa Bunge la Katiba.
Alisema ameshangazwa kuona kwamba yeye ndiye mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Taifa, Tanzania nzima na kushindwa kuteuliwa kuwa Mwakilishi katika Bunge la Katiba.
'Makosa haya kwa kiasi kikubwa yamefanywa na wenzetu Ikulu ya Zanzibar ambao hawakuwa makini kufuatilia na kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Kikwete'Alisema.
Aidha Soud alisema hakuna uwiyano wa nafasi za kushiriki Bunge la katiba ambapo Pemba imetoa jumla ya watu 8 tu huku Unguja zaidi ya watu 60 wakichaguliwa kuingia katika bunge la katiba.
Chama cha AFP kimeingiza jumla ya wanachama wawili katika Bunge la Katiba akiwemo katibu mkuu Rashid Mohamed kutoka Tanzania Bara.
-- via blogu za Zanzibar Islamic News na Lukwangule