Mwl. Mndeme: Wizi kwenye maduka ya nyama, Mwenge

Kwa wale mnaokwenda bucha kununua nyama munaelewa ni kwa jinsi gani nyama imepanda bei. 

Kwa sisi tunaogetemea bucha za maeneo ya Mwenge, tangu nyama ilipopandishwa bei mwezi December mwaka jana wakati wa sikukuu, hadi sasa haijashuka. Kilo moja ilipanda kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 7,000 huku stake ikipanda kutoka shilingi 6,000  hadi shilingi 9,000.

Pamoja na maumivu haya ya bei, kuna maumivu makubwa wanayopata wanunuzi wa nyama (hasa eneo hili la Mwenye) bila kujua kwa njia kuu mbili:
  • Moja ni kutobandikwa kwa bei ya nyama dukani na hivyo unapokuja kununua wakati wa kulipa wanakusoma iwapo unajua bei halisi au la na wanakupa bei ambayo sio halisi ukidhani ndio bei iliyoko. Wanakugundua zaidi pale utakapouliza bei kwa aina ya nyama unayohitaji.
  • Njia ya pili na kubwa zaidi, ningi ya bucha zilizoko pale zina mizani hii inayoonekana nzuri na ya  kisasa (kwa viwango vya Mwenge) kutokana na u-digitali wake. Hata hivyo mizani hii inatumika na wingi wa maduka haya ya nyama kuibia wateja kwa kiasi kikubwa sana bila wao kujua. 


Mizani hii inatakiwa ipime nyama ama ikiwa na sinia (kibebeo) kilichoko juu yake au pasipo kuwa nayo kulingana na unachopima. Hata hivyo, kwa vyovyote vile hapo kwenye weight inatakiwa isome 0.00 kabla ya kupima. Iwapo katumia Sinia inayoonekana kwenye picha kwa ajili ya kuwekea nyama, anatakiwa abadilishe calibration ili uzito wa sinia usiwe sehemu ya uzito unaopimwa. Hiyo sinia peke yake ina gramu 300 hadi 350 ambayo ni 1/3 ya kilo (zaidi ya robo kilo).
Wajanja hawa wa Mwenge kwa kuwa waanajua kuwa wengi hawana utaalamu wa vipimo, huwa wanaseti mizani kupima 0.00 kabla ya kuweka sinia na anapokuja kuweka sinia na nyama, ina maana nyama unayopewa ina gramu 700 au 650 badala ya 1000 kwa maana ya uzito wa kilo moja.Mizani hii inatakiwa ipime nyama ama ikiwa na sinia (kibebeo) kilichoko juu yake au pasipo kuwa nayo kulingana na unachopima. Hata hivyo, kwa vyovyote vile hapo kwenye weight inatakiwa isome 0.00 kabla ya kupima. Iwapo katumia Sinia inayoonekana kwenye picha kwa ajili ya kuwekea nyama, anatakiwa abadilishe calibration ili uzito wa sinia usiwe sehemu ya uzito unaopimwa. Hiyo sinia peke yake ina gramu 300 hadi 350 ambayo ni 1/3 ya kilo (zaidi ya robo kilo).
Wajanja hawa wa Mwenge kwa kuwa waanajua kuwa wengi hawana utaalamu wa vipimo, huwa wanaseti mizani kupima 0.00 kabla ya kuweka sinia na anapokuja kuweka sinia na nyama, ina maana nyama unayopewa ina gramu 700 au 650 badala ya 1000 kwa maana ya uzito wa kilo moja.