Nafasi ya bure ya mafunzo ya uigizaji filamu na uimbaji


RAFIKI ELIMU MUSIC & FILM ACADEMY
  • Je wewe ni kijana wa kitanzania?
  • Una umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea ?
  • Una ndoto za kuwa muigizaji filamu mkubwa nchini Tanzania?
  • Una ndoto za kuwa mwanamuziki ama muimbaji mkubwa hapa Tanzania ?
RAFIKIELIMU MUSIC & FILM ACADEMY ni kituo kinachotoa mafunzo ya UIGIZAJI na UIMBAJI kwa vijana wa kitanzania wenye umri wa kuanzia miaka kumi na tano na kuendelea.
 
Wahitimu wa mafunzo haya hupata nafasi ya kushiriki katika filamu , maigizo, tamthiliya na
nyimbo mbalimbali zinazo tayarishwa na Taasisi ya RAFIKIELIMU FOUNDATION.
 
ADA YA MAFUNZO : Mafunzo haya hutolewa BURE!
 
Mafunzo yataanza rasmi tarehe 02 MACHI 2014.
 
Mwisho wa kujiandikisha ni tarehe 28 FEBRUARI 2014.
 
Chuo chetu kinapatikana katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU mbele ya CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
 
Kufika Chuoni kwetu, panda daladala za UBUNGO-CHANGANYIKENI kisha shuka katika kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele, utaona bango limeandikwa RAFIKIELIMU FOUNDATION.
 
JINSI YA KUJIANDIKISHA :Tuandikie barua pepe kwenda : [email protected]
 
Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa SIMU 0784406508 Au Tembelea www.rafikielimu.blogspot.com