Nakala ya barua ya Madiwani waliojiuzulu CHADEMA

Zacharia Mfuko (kushoto) | Sebastian Peter Mzuka (kulia)

Madiwani wawili wa CHADEMA mkoani Shinyanga --wa Kata ya Ngokolo, Sebastian Peter maarufu Obama wa Ngokolo na Zacharia Mfuko wa Kata ya Masekelo -- wamejiuzulu nyadhifa zao walizokuwa wanazishikilia katika manispaa ya Shinyanga wakidai kuwa maamuzi yao yametokana na tuhuma walizozielekeza kwa Viongozi ngazi ya taifa wa chama hicho kuwa wanaendekeza majungu, migogoro, kudhalilisha baadhi ya viongozi pamoja na kuwapa majina ya wasaliti wa chama.

Hivyo wamesema wanalazimika kujiuzulu kama ishara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na
viongozi wa chama hicho Kitaifa.

Madiwani hao wawili tayari wameshakabidhi barua za kung’atuka nafasi zao katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga

Iliyopachikwa hapo chini ni nakala ya waraka wa diwani wa Ngokolo Sebastian Peter kuhusu suala hilo.

Nakala ya barua ya Madiwani kujiuzulu nyadhifa CHADEMA
(Bofya picha ili kukuza maandishi)


Nakala ya barua ya Madiwani kujiuzulu nyadhifa CHADEMA
(Bofya picha ili kukuza maandishi)

Nakala kutoka kwenye blogu ya malunde1


Jumatano ya Februari 25, 2013 waliokuwa Madiwani hao walitambulishwa rasmi mbele ya umati wa watu na Katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Shinyanga Mjini kuwa wamejiunga na CCM.