Launching of “Care for Me” campaign / NW, Kairuki azindua kampeni ya "Care For Me!"

DEPUTY Minister for Constitutional and Legal Affairs, Ms Angela Kairuki (left) cheers the launching of Care for Me Campaign at SOS Children’s Village in Dar es Salaam on Friday. The campaign aims at helping vulnerable children countrywide. Others (from right) are the Permanent Secretary in the Ministry of Community Development, Gender and Children, Ms Anna Maembe, SOS National Director, Anatoli Rugaimukamu, SOS Village Director, Angolwisye Mwollo-Ntallima, German Embassy Representative, Jan- Dieter Gosink and the Spouse of Turkish Ambassador in the country, Yesim Davutoglu. (photo: DAILY NEWS Staff Photographer)
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitia saini sehemu maalumu kutoa ujumbe wake mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine fedha zitakazopatikana katika kapeni hiyo zitahakikisha zinaongeza idadi ya vituo vya SOS kuwasaidia watoto yatima na waliopo katika mazingira hatarishi.


Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hizo za kuhamasisha jamii na makundi mbalimbali kuchangia na kumjali mtoto aliye katika mazingira hatarishi na yatima zinalenga kuwasaidia watoto zaidi ya 12,000 hadi kufikia mwisho wa kampeni yaani mwaka 2016.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Anna Maembe akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua kampeni.


Watoto wa Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam wakiwa kwene hafla hiyo.


Mkurugenzi wa SOS Tanzania, Mr. Anatory M. akizungumza na wageni waalikwa kabla ya uzinduzi.

 

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akiwa katika moja ya darasa la awali liloloendeshwa na Kijiji cha SOS, darasa hilo pia linatumiwa na watoto wa kawaida ambao hufundishwa pamoja na wale wa kituo hicho.

 

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akiwa katika moja ya darasa la awali liloloendeshwa na Kijiji cha SOS, darasa hilo pia linatumiwa na watoto wa kawaida ambao hufundishwa pamoja na wale wa kituo hicho.

 

Mwakilishi wa Kituo cha SOS kutoka nchini Kenya akizungumza na wageni waalikwa katika hafla za uzinduzi huo.


Burudani mbalimbali za ngoma na sarakasi kwa wageni waalikwa.

 

Meza kuu katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo.

 

Burudani mbalimbali kwa wageni waalikwa.


Ofisa Mkuu kutoka Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Ujerumani nchi Tanzania, Jan Dieter Gosink ambao ni moja wa wafadhili wa kituo hicho akizungumza na wageni waalikwa kabla ya uzinduzi wa kampeni za 'Nijali Mimi!' (Care For Me!) leo katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam.


Mratibu wa kampeni ya Care For Me kutoka SOS taifa, John Baptista akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo.

 

Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kijiji cha SOS wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Care For Me! iliyoandaliwa na kituo hicho.

 

Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kijiji cha SOS wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Care For Me! iliyoandaliwa na kituo hicho.

 

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Kairuki Azindua Kampeni Care For Me!


Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitembelea nyumba zinatumika kulala watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo.