Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili TBS Februari 2014

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wa nafasi za Inspection Technician II, Records Management Assistant II, Inspection Technician II (Deep sea) na Quality Assurance Officer II (Electrical Engineer) kuwa wafuatao wamechaguliwa kuendelea na usaili wa mahojiano utakaofanyika tarehe 25.02.2014
  • Kada ya Inspection Technician II, tarehe 26.02.2014 
  • Kada ya Records Management Assistant II na tarehe 27.02.2014 
Usaili utakuwa kwa kada za Inspection Technician II (Deep Sea) na Quality Assurance Officer II (Electrical Engineer).

Usaili utaanza saa 02:30 asubuhi katika ukumbi wa TBS ubungo Dar es Salaam.

Wasailiwa wanatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

1. Kuja na vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na vyeti vya taaluma

2. “Transcript”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita HAVITAKUBALIWA.

3. Kila msailiwa aje na kitambulisho kinachomtambulisha.

4. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

5. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanya usaili.

6. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa.

7. Usaili utaanza saa Mbili na Nusu asubuhi (02:30)

Bofya hapa kufungua faili lenye majina ya walioitwa kwenye usaili - Feb 2014.pdf