Picha za kikao cha NEC-CCM leo Jumapili


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili ukumbini kuendesha Kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma leo, Feb 16, 2014.


Wajumbe wa NEC, na Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakiwa ukumbini. Kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Feb 26, 2014. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Sheni


Sekretarieti ya Kikao Cha NEC ikiwa tayari kwa kazi ukumbini leo


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) akimsikiliza kwa Mzee Kazidi kutoka Kilimanjaro, wakati wakijadili jambo ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib 
Kwa picha zaidi za kikao hiki, bofya hapa