Picha za usiku wa Valentine’​s Day na Skylight Band @ Thai Village


Palikuwa hapatoshi....kama ulikosa juma lililopita basi burudani inaendelea leo pale pale Thai Village.


Lubea wa Skylight Band alitega mingo lango kuu la kuingilia na kugawa Shots za Tequila pamoja na Sambuka bure kwa wapenzi wa Skylight Band.Mashabiki wa Skylight Band wakipata shots za Tequila bure kwenye usiku maalum wa wapendanao uliofana Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.


Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye usiku wa wapendanao juma lililopita huku akisindikizwa na Mary Lucos, Sony Masamba na Sam Mapenzi.


Walipendezaje...: Digna Mbepera akifanya yake jukwaani.


MAJEMBE YA SKYLIGHT BAND....Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo katika hisia kali kwenye nyimbo za malavidavi huku akisindikizwa na Joniko Flower pamoja na Sony Masamba.


Birthday Girl....Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 (katikati) sambamba na Winfrida Richard pamoja na Digna Mbepera waking'ara kwa jukwaani kwenye usiku wa Valentine's Day juma lililopita.


Mheshimiwa Bundala anakwambia burudani ya Skylight Band ni Gym tosha, kama anavyoonekana pichani akisebeneka na mrembo.


Nakupenda pia...Nakupenda Pia...... Collabo ya Ukweeli kati ya Hashim Donode na Winfrida Richard njoo Ijumaa hii usikie kwa masikio yako.


Surprise.....Ilipotimia saa sita kamili ya kuamkia tarehe 15/2 alizaliwa Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47, waimbaji wenzake waliamua kumuimbia wimbo wa Happy Birthday na kumtakia maisha marefu.....Hujachelewa sana Ijumaa hii unaweza kum-wish belated Happy birthday na kazawadi kidogo....!
Champagne zilihusika na kufunguliwa na Mary Lucos pamoja na Sam Mapenzi.


Kuogeshwa nako kulihusika hajalisha umependezaje...lazima uoge kidogo....! Full Champagne....!!!

Kwa picha zaidi ingia bofya hapa