Rais Kikwete na Marais Wastaafu katika harambee ya kuchangia wodi ya dharura ya watoto na vifaa, Muhimbili

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa baada ya kuwasili katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. (picha: Ikulu)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa.

Mkurugenzi wa Radio One Bw. Deo Rweyunga akitangaza mchango wa makampuni ya IPP ya kununua kifaa cha thamani ya dola elfu 50

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa UNICEF nchini kwa mchango wa dola za kimarekani 100,000 huku Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa wakishuhudia.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bw. Lumbila Fyataga, mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Ikulu, kwa mchango wa kununua kifaa cha kuwapa joto watoto wachanga (Infant radiation warmer)  

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 toka kwa wawakilishi wa PPF ukiwa mchango wa mfuko huo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bi  Lucy Kimei kwa kuwasilisha shilingi milioni tatu kama mchango wa familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt Charles Kimei
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bi Lucy Kimei kwa kuwasilisha shilingi milioni tatu kama mchango wa familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt Charles Kimei

Rais mstaafu, Benjamin William Mkapa akimshukuru mwakilishi wa taasisi ya WAMA Bi. Caroline Mthapula kwa mchango wa taasisi hiyo