Shukurani za Asia Idarous Khamsin kwa kuiunga mkono "Lady in Red"

Asia Idarous akipita kwenye red Carpet
Asia Idarous akipita kwenye red carpet

MAMA wa Mitindo nchini na Mkurugenzi wa Fabak Fashins, Asia Idarous Khamsin amewashukuru wadau mbali mbali kwa kuendelea kulinga mkono onyesho la Mitindo la kila mwaka la 'Lady in red' ambalo kwa mwaka huu limeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake huku likiwa la mafanikio kwa kuibua wanamitindo wakubwa hapa nchini.

Akizungumza Dar es salaam, katika ofisi za Fabak zilizopo Msasani jirani na Kwa Mwalimu Nyerere, Asia Idarous alishukuru wadau mbali mbali waliojitokeza siku hiyo sambamba na wadhamini waliofanikisha kwa shughuli hiyo kubwa hapa nchini.

Asia alisema ni jambo la fadhira kwa kushukuru huku akiahidi kuboresha kama kulikuwa na mapungufu ya hapa na pale. "Muungwana ni vitendo, ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ ilikuwa ni ya kipekee kwa mwaka huu, hivyo nawashukuru nyote kwa kuliunga mkono jukwaa la Lady in red 2014, kwa kutimiza miaka hii 10" alisema Asia Idarous.

Na kuongeza kuwa, kuelekea onyesho la mwakani kwa mwaka 2015, jukwaa hilo la Lady in Red, linatarajia kuwa la kimataifa ikiwemo wabunifu wa kimataifa kuonyesha ubunifu wao hapa nchini.

"Kwa sasa tunaelekea anga za kimataifa kupitia jukwaa hili hili la Lady in red, zaidi ni kuendelea kuliunga mkono ilikutimiza ndoto hizi, na hii itasaidia kufungua milango ya wabunifu wetu kujiuza nje ya mipaka yetu" alisema Asia Idarous.

Onyesho hilo la Lady in red 2014, lililotimiza miaka 10, lilifanyika Februari 14, ndani ya ukumbi wa kisasa wa ndani ya hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Serena, ambapo siku hiyo pia ilikuwa ni maalumu kwa wapendanao duniani 'Valentine Day' watu wa kada tofauti wakiwemo mastaa na watu maarufu walijumuika kwa pamoja kuliunga mkono onyesho hilo.

Wabunifu mbali mbali wakiwemo magwiji na chipukizi walipata kuonyesha mitindo ya ubunifu kwenye jukwaa hilo na kuvutia wengi siku hiyo. mbali na ubunifu wa mavazi, pia liliendana sambamba na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, huku asilimia kadhaa za mapato yake yalipelekwa kusaidia waathirika wa dawa za kulevya.

Kwa upande wa burudani, wapendanao na wadau waliojitokeza walishuhudia burudani safi kutoka kwa wasanii mkali wa nyimbo za asili, Wanne Star na mkali wa R&B na Afro pop, Nemo ambaye hadi sasa anatamba na vibao mbali mbali ikiwemo My Number One, alichomshirikisha Omy Dimpoz.

Pia Asia Idarous aliwashukuru wadhamini wakuu, ikiwemo kinywaji cha Zanzi na Rasta za Darling. Wengine ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ya jukwaa hilo ni pamoja na Michuzi Blog, Vijimambo blog, Dj Bula, CXC, Times FM, Clouds Media, Michuzi Media Group, Channel TEN, Elite Computer, Eventlites, One Touch-Solution, Raysa Style, Paka Wear, Magic FM, DTV, Jambo Leo, i-View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.

Mbunge wa Bunge la Katiba, Mh. Maria Sarungi  akihojiwa na Deo wa Nivana wa East Afrika Television
Mbunge wa Bunge la Katiba, Mhe. Maria Sarungi  akihojiwa na Deo wa Nivana wa East Afrika Television

Mmiliki wa Michuzi Media Group, Mr. Michuzi na mkewe
Mmiliki wa Michuzi Media Group, Mr. Michuzi na mkewe

Asia akiwa na mumewe jukwaani, kushoto ni Miss Universe
Asia akiwa na mumewe jukwaani, kushoto ni Miss Universe

Msanii Nemo akilitawala jukwaa
Msanii Nemo akilitawala jukwaa

Martin Kadinda miongoni mwa wabunifu waliopata mafanikio kupitia jukwaa la Lady in Red
Martin Kadinda. miongoni mwa wabunifu waliopata mafanikio kupitia jukwaa la Lady in Red

---
Habari imeandikwa na kuwasilishwa na Andrew Chale; Picha: Michuzi blog.