Taarifa ya Alex Kassuwi: Upotofu na uharibifu wa Augustino Malinda na Dickson Mkama

Ndugu zangu asanteni kwa kunipigia simu nyingi sana na kunitakia kheri. Nilikuwa safarini. Asanteni kwa support.

Ninatoa tamko la kupinga na kukanusha taarifa za upotofu na uharibifu wa Augustino Malinda na Dickson Mkama.

Mimi bwana Alex Kassuwi mmiliki wa Swahili Tv ninakanusha habari za upotofu kwa jamii na uharibifu uliokusudiwa kunichafua kwa upuuzi kabisa. Habari zilizotolewa siyo za kweli.

Chanzo cha yote ni kudai haki zangu katika Swahili Tv na haki za watoto wangu katika wizi uliofanywa na bwana Augustino Malinda kuiba hela za michango ya msiba na tamaa za
bwana Dickson Mkama.

Kwanza napenda umma uelewe kwamba mimi bwana Alex Kassuwi ndiyo mmiliki halali wa Swahili Tv na Swahili Tv blog na document zote ninazo. Nilianzisha na kusajili kihalali kwa kufuata taratibu zote za kisheria kampuni yangu Swahili tv na kampuni zingine tanzu hapa Marekani zamani hata kabla sijamjua na nilikuwa sijawahi kukutana na bwana Augustino Malinda na bwana Dickson Mkama.

Swahili Tv mbali na kuweka vipindi online, inazalisha na kuuza vipindi katika
tv zingine, hapa awali nikiwa peke yangu niliweza kuandaa vipindi mbalimbali vingine vikiwa online na vingine vingi havijatoka bado viko mitamboni.

Swahili tv ilianza kufanya vipindi maarufu vya mahojiano mbalimbali na kuwa na kipindi cha weekend special kutokea hapa Washington DC. Malengo yangu ya
kuanzisha Swahili Tv na Swahili Tv blog hapa marekani ni kuitangaza Tanzania na kuiletea sifa nchi yangu, kuendeleza lugha ya Kiswahili na kudumisha mahusiano na watu wa Marekani kijamii, kitamaduni, kibiashara na burudani.

Kuanza na kufa kwa MMK Mmedia Group

Baada ya muda mrefu kupita nikiwa mwenyewe nikakutana na Augustino Malinda na Dickson Mkama. Nilifanya kosa kubwa kufanya ubia na watu nisiowajua background zao. Tukaanzisha MMK Media Group.

(M=Malinda, M=Mkama, K=Kassuwi). Tukiwa MMK Media Group tulijitangaza sana, tulitambulika hivyo kwa jamii, ubalozini na katika vyombo mbalimbali vya habari.

Makucha ya Augustino Malinda na Dickson Mkama yakajionyesha muda mfupi sana. Nikaona maono/vizion yangu na wao ni tofauti mapema. Hawa watu siyo waaminifu na wanapenda sifa za kijinga, na maboblishi yasiyo na maana, kujikweza kwa kijinga.

Augustino malinda alisema anafanya kazi DC Tv na akaahidi kuwa Swahili Tv itakuwa inaonekana live pale DC Tv. Mimi muda mfupi nikagundua kuwa Augustino Malinda siyo mfanyakazi wa DC Tv na tayari kesha niingiza mkenge. Nikiwa MMK Media Group nili-injinia Swahili radio online tuliweza  kufanya matangazo bila
kuwa na ofisi, tulifanya kutokea nyumbani kwangu kisha nyumbani kwa Dickson Mkama.

Swahili radio na MMK Media Group hajiwahi kusajiliwa popote pale na haijawaji kuwa na ofisi wala vifaa vya kazi, wala akaunti katika benki yoyote ile.

Mbali na MMK Media Group kutokuwa na vifaa vya kazi na fedha, tuliendesha MMK Media Group kutoka katika mifuko yetu pesa zetu binafsi, tulikuwa tukikodi studio na vifaa toka sehemu nyingine kufanyia kazi za MMK Media Group na ushahidi upo.

Kutokana na sifa za hawa ndugu kuwa mbaya katika jamii na misifa isiyo na msingi, ikawa ngumu kwa mimi kupiga hatua na mbaya zaidi hata mimi  mwenyewe kunitapeli.

Swahili Media Group ni kitu gani?

Katika muda mfupi tuliokaa pamoja kila siku nilishauri tuisajili hii kampuni ya MMK Media Group kisheria hapa Marekani, lakini bwana Augustino Malinda na Dickson Mkama wakanizunguka mchana kweupe na kuanzisha kampuni ambayo mimi siijui na siielewi inayoitwa Swahili Media Group. Baada ya kuomba maelezo kwa nini
wameamua hivi na kushindwa kutoa majibu, wakawa wananikimbia ndipo nikamua kujiondoa na umoja huu wa mashaka.

Watazamaji wetu mtakumbuka tulijitambulisha katika umma kuwa sisi ni MMK Media Group.  MMK Media Group haikuwahi kusajiliwa popote pale. Ni mimi pekee bwana Alex Kassuwi ndiye niliyesajili Swahili Tv na jina la SwahiliTv nembo hapa Marekani. Ndiyo sababu nilijiengua na bwana Augustino Malinda na Dickson Mkama baada ya kunitapeli.

Mbali na sifa zao kuwa mbaya, hawana ujuzi katika television na teknolojia ya kuendesha mitambo kama walivyonidanganya hapo mwanzo, ndipo nilipoamua kuachana nao rasmi. Nilipowapa tamko rasmi la kuachana nao haraka wakaiba passowrd ya blog yangu na kuibadili. Na kuanza kuitumia hiyo blog kunichafua mimi.

Si kweli. Ni uzushi wa kijinga, Nakanusha uzushi na upuuzi wa bwana Augustino Malinda na Dickson Mkama kuwa nilibadhirifu ama eti kuiba mali zenye thamani ya $15,000. Habari hizi si kweli na ni uongo wa kunichafua. Hizi sifa za kijinga.

Katika umoja wetu wa MMK Media Group, narejea tena, hatukuwahi kumiliki ofisi wala vifaa vya uzalishaji vipindi. Vifaa vyote tulivyotumia tulikuwa tunaazima na kukodi kutoka sehemu mbalimbali. Nilitumia vifaa toka chuo ninachosoma na ushahidi upo na pia tulikodi vifaa toka sehemu mbalimbali.

Bwana Augustino Malinda na Dickson Mkama hawana vifaa vyoyote vya kuzalisha vipindi wala ujuzi. Ninachojua, wanakodi, na hata ofisi hawana. Na kama wamepata vifaa na ofisi itakuwa jana.

Augustino Malinda na Dickson Mkama acheni mambo ya kipuuzi, yinyi ni watu wazima na mna familia. Hata wake zenu wanajua nyinyi ni waongo, na hela hamna.

Kifupi Augustino Malinda na Dickson Mkama siyo watu waaminifu, wana credit chafu katika jamii yetu. Nilishauriwa sana kuachana na hawa watu lakini nilijua wamebadilika lakini kumbe bado ni matapeli. Wametunga na kuzusha habari hii ili kunichafua hasa baada ya kuindoa Swahili Tv katika ushirika wao.

Hawa watu wanaweza kuua mtu! Wewe fikiria Swahili Tv ambayo haijaanza kuingiza mapato na SwahiliTv blog amabayo pia haina mapato, haina hela, haina vifaa, haina ofisi, tumekuwa tukiandika habari na kuweka picha kama hobby wanazusha uongo huu!! Hawa ni watu hatari sana. Nawajua watafoji, watafanya chochote hata wata fake document ku-support uzushi wao. DMK ameshafungwa jela kwa wizi na ku-foji/ ku-fake nyaraka hapa Marekani na ushahidi upo.

Nitachambua kwa kina double faces za Augustino Malinda na Dickson katika post ijayo na vituko walivyonifanyia toka nimewajua.

Usikose kusoma na pia kumshirikisha mwenzako ili kuweka kila kitu wazi. Kama hupendi dhuluma tafadhali share na like hii post.

ALEX KASSUWI