Taarifa ya mafanikio ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN) UNAFANYAKAZI
“Mabadiliko katika mfumo wa Serikali katika utendaji kazi kupata mafanikio haraka”

Dar es Salaam, Tarehe 5 Febuari, 2014: Ofisi ya Rais - Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa umma kuwa utekelezaji wa mfumo wa – Big Results Now ! (BRN) unaendelea vizuri. Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miradi katika maeneo sita ya kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu, Maji, Nishati , Uchukuzi na
Utafutaji wa Rasilimali). Mfumo wa BRN unaweka wazi malengo pamoja na kuainisha uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi katika utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.

Kila Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU)) ambacho kinafanya kazi kwa karibu sana na OR-UUM. Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za kila wiki na mwezi ambazo huwasilishwa OR-UUM. Taarifa za MDU zinajadiliwa kila mwezi kwenye mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia eneo la kimkakati Kitaifa (Steering Committee Meetings) ambayo Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja na Baraza la Mageuzi na Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mikutano hii inalenga kutatua changamoto au vikwazo vilivyojitokeza.

Aidha, Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs) ili kuongeza ufanisi wa kutekeleza miradi katika ngazi zote.

Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo yaliyolengwa. BRN inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya uwajibikaji katika ngazi zote za utumishi wa umma.

Ili kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi ambayo italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji. Ili kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa kurazinisha mfumo na taratibu za ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba sekta binfasi inatoa mchango wake stahiki katika kutekeleza BRN

MWISHO
Kuhusu Matokeo Makubwa Sasa (BRN):
BRN ni usimamizi utendaji unao tafsiri mipango ya miradi ya maendeleo kuwa mipango yenye tija kwa sababu ya malengo yaliyopangwa kufanya watendaji kuelewa wajibu wao vyema na kutambua kirahisi nani na maeneo ambayo hakuna uwajibikaji katika utekelezaji wa mradi.

Maeneo sita ya kimkakati kitaifa yaliyochaguliwa na kuridhiwa na Baraza la Mawaziri kufuatia mikutano kadhaa maalum ni:


1. Usambazaji wa maji salama vijijini - Wizara ya Maji

2. Ulinzi wa Chakula – Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

3. Elimu ya msingi na sekondari – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

4. Kumiarisha usafirishaji wa Bandari, Reli na Barabara katika kanda ya kati – Wizara ya Uchukuzi

5. Upatikanaji and Uzalishaji – Wizara ya Nishati na Madini

6. Kuziwezesha kifedha miradi katika mfumo wa MMS – Utafutaji wa rasilimali fedha (Fedha)- Wizara ya Fedha

Kazi ya OR-UUM kusaidia, kuwezesha, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa MMS katika maeneo sita ya kimakakati kitaifa kwa njia ya mawasiliano na ufumbuzi wa matatizo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari imetolewa na: OR- UUM Mawasiliano, tafadhali wasiliana na OR- UUM kwenye:  ([email protected]) or +255 658 870010 kwa maelezo zaidi au ufafanuzi.