Taarifa ya Ofisi kuhusu kurasa zenye jina la Lowassa katika mitandao jamii

Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mhe. Edward Lowassa katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram n.k. zinaonekana mmiliki wake ni Mhe. Edward Lowassa.

Ukweli ni kwamba hizo zote hazimilikiwi na Mhe. Lowassa.

Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo
hazihusiani kwa namna yoyote na Mhe. Lowassa.

Hata hivyo Mhe. Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (MB)