TANESCO yapokea mitambo ya kuzalishia umeme

Moja ya mitambo ya kuzalishia umeme ikipakiwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda Kinyerezi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi wa tatu na kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam jana ambapo mitambo hiyo imepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi.

Habari na gazeti la UHURU, picha na Benjamin Sawe/Maelezo -- SERIKALI imepokea mitambo miwili ya kuzalisha umeme wa megawati 75 kwa ajili ya mradi wa Kinyerezi I ambao unatarajiwa kukamilika Oktoba, mwaka huu.

Mitambo hiyo kutoka Marekani, ilipokewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, ambaye alikuwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, katika bandari ya Dar es Salaam.

Maswi alisema mradi wa Kinyerezi I utazalisha megawati 150 na kwamba mitambo hiyo ni ya awamu ya
kwanza ambayo itakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 75.
"Serikali tunatekeleza ahadi tulizozitoa kwa wananchi katika kupunguza ghrama za uzalishaji umeme. Meli hii kubwa ina shehena ya mitambo ya kuzalisha megawati 75 ambayo tutaisimika Februari 28, mwaka huu"
alisema.

Alisema mitambo hiyo haitakuwa na athari kwa kuwa ni ya kisasa na awamu ya pili itawasili nchini mwezi ujao. Mitambo hiyo imetengenezwa na kampuni ya General Electric.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi (kushoto) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi Mramba wakati wa halfa ya kupokea mitambo miwili ya kuzalisha umeme yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 183 itakayokwenda kufungwa Kinyerezi ambapo mitambo hiyo itaanza kufanya kazi mwezi wa kumi mwaka huu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Mramba, alisema kuwasili kwa mitambo hiyo ni hatua za msingi za kutatua tatizo la umeme nchini, ambapo tangu uhuru uwekezaji wake ulikuwa duni.
"Katika historia ya nchi tangu Uhuru hatujawahi kuwa na uwekezaji mkubwa kama huu. Mitambo ya kuzalisha umeme itatatua suala la uzalishaji umeme hivyo bado usafirishaji na usambazaji. Watanzania tuna mipango mingi inayotekelezeka jitihada za leo (jana) ni sehemu ya mipango hiyo"
alisema.

Mhandisi Mramba alisema katika eneo la Kinyerezi kuna miradi minne ambayo ni Kinyerezi I, II, III, IV ambayo itapunguza matatizo ya uzalishaji umeme.

Aliwaomba Watanzania kuwa na subira kwa kuwa matatizo ya umeme yatafika mwisho kutokana na miradi mikubwa iliyopo ambayo utekelezaji wake ni wa makini na madhubuti.

Kwa upande wake, Meneja wa Miradi ya Uzalishaji Umeme TANESCO, Mhandisi Simon Jirima, alisema mitambo hiyo itahifadhiwa katika eneo la mradi na baada ya uzalishaji, umeme utaingizwa kwenye gridi ya taifa.

Mhandisi Jirima alisema mradi huo utagharimu dola za Marekani milioni 183 (zaidi ya sh. bilioni 250).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi akishuka kutoka juu ya meli wakati wa Hafla ya kupokea mitambo miwili ya kuzalishia umeme thamani ya Dola za Kimarekani milioni 183 kutoka kwenye Kampuni ya General Electronics ya Marekani inayokwenda kufungwa Kinyerezi,hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam jana.