Tangazo la nafasi za kazi 517 Serikalini


Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza jumla ya nafasi wazi za kazi 517 kwa ajili ya waajiri mbalimbali nchini.


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amewataka waombaji wote wa fursa za ajira serikalini kuzingatia masharti ya tangazo, ikiwa ni pamoja na kuambatisha vielelezo muhimu kabla ya kutuma barua ya maombi. Aidha, amesema nafasi hizo za kazi zimewekwa katika tovuti Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz. Ambapo ali bainisha kuwa ya mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 03 Machi, 2014.

Daudi amesema nafasi zilizotangazwa kuwa ni nafasi ya Afisa lishe, Msaidizi lishe, Mlezi wa watoto msaidizi, Afisa ustawi wa jamii, Msaidizi ustawi wa jamii, Mhudumu wa jikoni/mess, Afisa misitu, Msaidizi misitu,
Mkufunzi kilimo, Mhandisi kilimo, Muunda boti, Dereva wa vivuko, Afisa mifugo, Mhasibu msaidizi, Afisa ushirika, Afisa ugavi, Afisa ugavi msaidizi na Afisa utamaduni.

Wengine ni pamoja na Afisa maendeleo ya vijana, Afisa ufugaji nyuki, Afisa ardhi, Fundi sanifu kompyuta, Afisa biashara, Msaidizi wa hesabu, Afisa usimamizi wa fedha, Afisa tarafa, Afisa wa Sheria, Fundi sanifu– ramani, Fundi sanifu - urasimu ramani, Fundi sanifu, Afisa wanyamapori na Afisa michezo.

Daudi alibainisha kuwa nafasi hizo zilizotangazwa ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wakiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Rukwa na Katibu Tawala Mkoa Njombe.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba.

Amesema nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Katibu alifafanua kuwa nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
Katibu amewahimiza waombaji wa nafasi za kazi Serikalini kujiandaa vyema pindi wanapopata fursa ya kuitwa kwenye usaili ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kupata kazi wanayoomba.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 17 Februari, 2014