Ushauri
huwa na lengo la kuzuia tatizo lisitokee, hivyo mara nyingi ushauri hutolewa kabla ya tatizo kutokea. Wakati wa ushauri, mteja (mshauriwa) huwa ni mpokeaji tu wa ushauri toka kwa mtoa ushauri. Mshauri anaweza kuwa ni mtu yeyote. Hivyo kwa ujumla, Ushauri hutolewa kwa mtu yeyote.
Nasaha (Unasihi)
hutolewa baada ya tatizo kuwa limetokea. Mara nyingi nasaha hutolewa kwa lengo la kutibu au kupunguza uwezekano wa tatizo lililopo kutokea tena au kumfanya mwenye tatizo akubaliane na hali halisi kuwa analo tatizo na kuangalia namna ya kukubaliana na kukabiliana nalo. Wakati wa Unasihi, mtoa nasaha (Mnasihi) na mteja (mnasiwa) hubadilishana mawazo na si mpokeaji tu wa kile kinachopendekezwa na mnasihi. Unasihi hutokana na kujifunza na kuwa mtaalamu wa kutoa nasaha.Hivyo, unasihi hutolewa kwa mtu mwenye tatizo tu.
Mtembelee Mwalimu Gunda kwa maarifa zaidi ya Ualimu kama vile Maswali na Majibu | Dhana ya Ualimu na Makazi ya Maarifa | Nadharia za Kujifunza katika tovuti ya jiandae.com