Togolani Mavura ateuliwa kuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba)

Togolani Mavura
Togolani Mavura

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Togolani I. Mavura kuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) kuanzia Februari 8, mwaka huu, 2014.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Februari 25, 2014, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Bwana Mavura anachukua nafasi ya Bwana Msafiri Marwa ambaye amehamishimiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kupangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mavura ambaye ni Ofisa wa Mambo ya Nje alikuwa Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

“Mwisho”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

25 Februari, 2014