Mwandishi wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakina mama wengi Afrika. Kati ya mwaka 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na kubadilisha historia katika kizazi cha leo.
Katika shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.
Maonyesho hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.
Na sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa duniani.

![]() |
Mmoja wa wananfunzi akibadilishana mawazo na Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet anayetumia maonyesho ya picha mbalimbali kuelimisha jamii kupitia picha hizo. |
Ujumbe unasema kwamba ukeketaji umepungua katika sehemu kubwa ya dunia na takwimu zinasema kwamba zaidi ya wanawake na wasichana 125 milioni ambao wanaishi katika dunia ya leo katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya kati walifanyiwa vitendo vya ukeketaji, na kama swala hii likiendelea zaidi ya wasichana 86 milioni duniani watafanyiwa vitendo vya ukeketaji kufikia mwaka 2030.
Baadhi ya picha za wanawake nchini Tanzania ambao wameleta mabadiliko katika maisha yao na wengine hapa nchini.
Baadhi ya picha zinazoonyesha matukio mbalimbali yaliyokusanywa na Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet.
