[video] Rais Kikwete azungumza na BBC kuhusu vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori

Mwanamfalme wa Uingereza, Prince Charles na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron ni miongoni mwa wenyeji wa mkutano wa kimataifa unaofanyika jijini London, ukilenga kuzuia uwindaji wa wanyama walio hatarini kutoweka duniani.

Biashara hiyo yenye kuingiza takribani Dola za Kimarekani bilioni 19 kwa mwaka, imeenea kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya pembe za ndovu nchini Vietnam na China.

Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amezungumza na  Mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuhusu janga hilo linaloikumba nchi hiyo na namna Serikali inavyokabiliana nalo.

Bofya kifute cha pleya iliyopachikwa hapo chini kutizama video hiyo.