![]() |
Muonekano wa duka jipya la Vodacom lililopo Tabata Magengeni.Duka hilo linatarajiwa kuwarahishia wateja kupata huduma kwa karibu na kuwapunguzia usumbufu na gharama za kufuata huduma umbali mrefu. |
Dar es Salaam, 23 Februari 2014 -- Wateja wa Vodacom wameendelea kukumbushwa kupata huduma katika maduka mapya yanayoendelea kufunguliwa maeneo mbalimbai karibu na makazi ili kuepuka gharama na usumbufu usio wa lazima wa kufuata huduma kwenye maduka yalyozoeleka yaliyopo mjini na yaliyo kwenye maeneo ya kibiashara.
Vodacom kwa sasa imekuwa ikifungua maduka sehemu mbalimbali ili
kuwapunguzia gharama na muda wateja wake ikiwemo lilifunguliwa jana Tabata Magengeni jijini dar es salaam duka ambalo litatoa huduma kwa wakazi wa maeneo ya Tabata.
Mkuu wa idara ya Mauzo ya Rejareja wa kampuni hiyo, Upendo Richard amewataka wateja hao kutumia ipasavyo duka hilo na kuachana na kuepuka adha kusafiri kwenda mbali kutafuta huduma za Vodacom kwani duka hilo litakuwa likitoa huduma zote wanazo hitaji wateja wa kampuni hiyo.
“Huduma katika maduka yetu yote bila kujali eneo lililopo yanatoa huduma zenye ubora sawa na za kiwango cha juu. Alisema Upendo na Kuongeza "lengo letu ni kuwasogezea wateja huduma karibu na walipo hivyo tunawaomba wayatumie kwa kujiamini na watapatapa suluhusho la mahitaji yao yote"aliongeza Upendo.
Kwa Upande wao wakazi wa Tabata Bwana, Saimon Edward Rugenga na Bi. Arafa Hamza ambao ni wateja wa kwanza kupata huduma katika duka hilo wamesema kusogezwa kwa huduma kwa wateja katika maeneo hayo ni jambo jema kwani sasa wateja wa matandao huo hawatopata tena tabu ya kusafiri kutoka tabata kwenda maeneo mengine ya mji kufuata huduma hiyo.
“Eneo hili la tabata Magengeni ni eneo la makazi ya watu, tumezoea kuona maduka kma haya yakijengwa sehemu zenye maofisi au biashara, sasa kwa hatua hii ya kutuletea huduma hasa watu tulioko maeneo ya pembezoni mwa mji ni jambo jema ninaamini duka hili litatusaidia wakazi wengi na ninawasihi Vodacom wasiishie hapa Tabata waendelee katika maeneo mengine ya Mikoani,” alisema Bwana, Saimon Rugenga.
Nae Bi Arafa Hamza alisema “Kwa kipindi kirefu wateja wa Vodacom walioko tabata na maeneo ya karibu walilazimika kwenda buguruni, posta au Mlimani city ili kufuata huduma sasa jambo hili halitokuwepo tena, na yeye kama mfanyabiashara atakamilisha mahitaji yake yote ya kimawasiliano katika duka hilo, alisema na kuhitimisha kuwa” Hatua hii ni yakupongezwa na watoa huduma za mawasiliano wengine waige mfano huu ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma hizi za mawasiliano kwa Watanzania.” Alisema.
Duka hilo ambalo ni la 77 kufunguliwa nchini litakuwa likitoa huduma mbalimbali zikiwemo ununuzi wa modem, kusajili laini, kuunganishwa na intaneti, kufanya manunuzi ya simu, huduma mbalimbali za M-Pesa pamoja na ushauri wa huduma za kimawasiliano.