Wakali wa vitafunwa jijini Dar es Salaam - The Ladies

 Joan Joseph Massawe (kulia) na Angel Fabian Massawe
 Joan Joseph Massawe (kulia) na Angel Fabian Massawe

Na Mroki Mroki -- Ujasiriamali ni jambo lililojema miongoni mwa jamii. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kukosa vitu vya kufanya ili kuweza kujipatia kipato na kuacha kuwa tegemezi kwa wazazi au waume na hata wakati mwingine wake zao. 

Wanadada wawili marafiki ambao kwa bahati majina ya ubini ya wazazi wao yanafanana na wao kuamua kujiita ndugu, Joan Joseph Massawe (pichani kulia) na Angel Fabian Massawe wao kwa kuliona hilo waliamua kuanzisha bishara ambayo itawapatia kipato cha ziada mbali na ajira zao nma kuwasaidia katika masomo yao.

Wakiuambia mtandao wa Father Kidevu Blog kuwa wao ni wasomi na wameamua kuopika vitafunwa vya aina mbalimbali na kuviuza na pia wamekuwa wakifanya hivyo katika
tafrija mbalimbali kwa kupika bite.

Muiongoni mwa vitu ambavyo leo viilivuta FK Blog hadi katika meza ya wana dada hao 'The Ladies' iliyopo katika maonesho ya Tamasha la Mwanamke na Akiba ndani ya Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam ni vitumbua. Yes vitumbua hivi hivi, maana ni vikubwa na vina mvuto. Lakini pia katika meza yao kulikuwa na vitu vingi kama chapati za kumimina na kusukuma, sambusa, kababu, na kalimati.

Wanadada hawa ni mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo waliamua kubuni biashara hiyo. Ni wazi kuwa hata hapo baadaye wakiwa na kampuni kubwa ya biashara hii sitaweza kushangaa.


Pichani ni Angel na Joan wakiwahudumia wake wa viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais mama Asha Bilali aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha la Mwanamke na Akiba.Angela na Joan wakimhudumia mama Asha Bilali vitumbua hivi ambavyo leo navizungumzia. Hakika kila mama aliyepita katika banda hilo hakuacha kununua kitafunwa.
Vitumbua hivyoooo kazi kwenu wana dada hawa wanapatikana Oysterbay barabara ya Bongoyo. 

MAWASILIANO ZAIDI KWA WENYE UHITAJI: 

+255 713 185065 AU +255 652 035652