Wakuu wa Mikoa wapongezwa kwa kuhamasisha uwekezaji Kanda ya Ziwa
Mikoa ambayo itashiriki katika Kongamano la Uwekezaji la Kanda ya Ziwa ni Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga Kongamano ambalo kwa pamoja litawakutanisha Wawekezaji pamoja na
Serikali katika kujadili vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana katika mikoa hiyo ya kanda ya Ziwa.
Kituo cha Uwekezaji Kimejizatiti kushirikiana na Mikoa katika kuhakikisha kuwa wawekezaji wanapatiwa huduma zinazohitajika katika Mikoa.
Kituo cha Uwekezaji na Mikoa wamekubaliana kushirikiana na kuhakikisha kupatikana kwa Ardhi katika Mikoa ili iweze kuwekwa kwenye Benki ya Ardhi kwa ajili ya kupatia Wawekezaji na pia kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu sheria na taratibu zinazomtaka muwekezaji kuzifuata kabla ya kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Kituo cha Uwekezaji pia kitafanya kazi na Makatibu Tawala wa Mikoa ili kujenga uwezo ili nao waweze kusimamia utoaji wa huduma vizuri kwa wawekezaji katika mikoa yao.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Kongamano la Uwekezaji Tanga na Vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana Kanda ya Ziwa tembelea tovuti ya www.lakezoneinvestmentforum.go.tz