Washindi waendelea kubeba bodaboda zao kutoka Vodacom

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifurahi na Mama Domotila Charles akikwaa bodaboda yake tayari kuiwasha na kuondoka nayo kutoka Makao Makuu ya kampuni hiyo akiwa ni mmoja wa washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda iliyomalizika hivi karibuni.


Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifafanua jambo kwa mmoja wa washindi wa Bodaboda Amanzi Mohamed kutoka Bagamoyo wakati wa zeozi la washindi hao kuchukua bodaboda hizo Makao Makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es salaam.Washindi hao ni wa Promosheni ya Timka na Bodaboda iliyomalizika hivi karibuni.


Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (wa pili kushoto) akiwaruhusu washindi wa iliyokuwa promosheni ya Timka na Bodaboda kuondoka na bodaboda zao mara baada ya kuzipokea rasmi makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.


Ofisa Masoko wa Vodacom Prestin Lyatonga na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim wakiwaanga washindi wa bodaboda wa iliyokuwa promosheni ya Timka na Bodaboda. Iliyomalizika. Washindi mbalimbali wanaendelea kuchukua zawadi zao hizo kutoka Makao Makuu ya Vodacom jijini Dar es Salaam.