- Shule 12 kutoka wilaya tatu za mkoa huo kutoana jasho
Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa na ya aina yake yatahusisha shule kumi na mbili za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam kutoka wilaya zake tatu; kwa wilaya ya
Kinondoni shule zitakazoshiriki ni Turiani, Mugabe, Kawe na Kiluvya; Ilala ni Benjamini William Mkapa, Mnazi Mmoja, Majani ya Chai na Juhudi; Temeke ni Kibasila, Temeke, Pendamoyo na Mtoni Relini.
Mashindano hayo yanaanza kutimua vumbi kuanzia Februari 8 na kuhitimishwa siku ya tarehe 23 ya mwezi huu. Viwanja vitakavyotumiwa ni vitatu yaani kimoja kutoka kila wailaya ambavyo ni Kibasila (Temeke), Benjamini Mkapa (Ilala) na Turiani (Kinondoni).
Akizungumza wakati wa mashindano hayo mheshimiwa waziri Dk. Fenella Mukangara alibainisha kuwa ni kwa muda mrefu sasa michezo mashuleni imekuwa ni ya kusuasua kitu ambacho kinapelekea vipaji vya wachezaji wachanga kutoonekana.
“Ni muda sasa tangu michezo mashuleni kama vile UMITASHUMTA kufanyika, kipindi kile michezo ya aina mbali mbali kama vile mpira wa miguu, netiboli, riadha na mingineyo ilikuwa ikiwakutanisha wanafunzi na kuonyesha vipaji vyao. Tunataka kurudisha hayo mashindano kama ilivyokuwa zamani, naamini kwa kushirikiana na wizara husika pamoja na wadau mbali mbali lengo letu tutafanikiwa.” Alisema Dk. Mukangara
Aliongezea kwa kusema mashindano haya yatafungua njia na kurudisha ari ya wanafunzi kupenda michezo na kuwa ni sehemu ya masomo yao. Hatutaki iwe ni nadharia tu kwamba michezo ni muhimu kwa afya ya mwili na akili.
“Kwa kuanza na shule hizi chache za mkoa wa Dar es Salaam tunaamini mashindano yatakuwa ni yenye msisimko na ushindano mkubwa na tunategemea zoezi hili kusambaa mikoa tofauti ya Tanzania. Ningependa kutoa rai kwa shule zilipata fursa ya kushiriki kuitumia nafasi hiyo ipasavyo, nawatakia maandalizi mazuri, mtuonyeshe soka safi na hatimaye kuibuka na ushindi.” Alimalizia mheshimiwa waziri
Mashindano hayo maalum kwa ajili ya shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam yamedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ambapo walitoa vifaa kama vile jezi, mipira na gharama za uendeshaji kwa kila timu pamoja na kikombe kwa timu itakayoibuka mshindi.
Kwa upande wake akizungumza wakati wa ufunguzi huo Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salum Mwalim amesema kwa upande wao michezo ni kitu muhimu katika jamii yetu na inapendwa na kila mtu hivyo ni jambo jema kuunga mkono jitihada hizo.
“Kampuni ya Vodacom imekuwa ni mdau mkubwa wa michezo nchini na tunashirikiana bega kwa bega na serikali kuhakikisha sekta hiyo muhimu inakua nchini. Kampuni ndiye mdhamini wa ligi kuu Tanzania bara kwa muda mrefu sasa hivyo sasa tunataka tuanzie kuibua vipaji huku ngazi za chini kabisa ili kuja kupata wachezaji bora wataoipeperusha vema bendera ya taifa letu.” Alimalizia Bw. Mwalim.