Yericko Nyerere: Kwa nini Nyerere ali-veto kumkataa Lowasa?

Kwa nini Hayati Baba wa Taifa alitumia kura yake ya veto kumkataa Lowasa kwa sababu iliyoitwa na inayoaminika mpaka sasa kuwa “Lowassa ana utajiri mkubwa usio na ufafanuzi alioupata kwa mda mfupi tu akiwa mkurugenzi wa AICC?”

Ikumbukwe ni kuwa hoja hiyo ya Mwalimu Nyerere ilikuja baada ya Lowassa na wapambe wake kukodi ndege binafsi kutoka Arusha kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya uteuzi wa urais mwaka 1995, kitendo
 hiki kilimfedhehesha sana Mwalimu na wazalendo wengine na hata kufikia kuliondoa jina la fisadi huyu nguli wa Tanzania,

Je leo utajiri wa Lowassa umekuwa halali?

Mamlaka ya mapato Tanzania inaweza kututhibitishia uhalali wa kodi alipayo mtu huyu?

Tangu afukuzwe uwaziri mkuu mwaka 2007 taarifa za kuaminika kutoka vyanzo muhimu nikuwa Lowassa alitenga Tsh12 bilioni kwa ajili ya kujitakasa, ambapo mpaka leo hii ameshatumia Tsh8 bilioni, je pesa hii ameipata wapi? Imelipiwa kodi kiasi gani? Atairudishaje akiwa rais?

Ili kuhuisha mjadala huu hebu niwaeleze jambo muhimu dhidi ya mtu huyu aitwae Edward Ngoyai Lowasa,

Labda niwaelekeze watafiti watafute faili la EL la enzi za TANU pale Lumumba. Mzee Paul Sozigwa suala hili analifahamu fika.

Ndiyo, Mwl. Nyerere alichukizwa na tabia ya Lowasa ya kujitajirisha kwa kuiba mali ya umma. Lowasa, licha ya tuhuma za wizi enzi akiwa AICC, kujimilikiaha majumba ya Masajili wa Majumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Mwl. Nyerere alikuwa akifahamu wizi wa Lowasa tangu enzi za TANU. Kati ya mwaka 1974 na 1977 Lowasa aliiba pesa za TANU alizopewa kusamia ujenzi wa ofisi ya TANU Arusha.

Badala ya kujenga ofisi ya TANU Lowasa alinunua kiwanja na kujenga nyumba yake binafsi. Jambo hilo lilipogundulika mwaka 1982, lilimkasirisha sana Mwl hivyo kuamuru afukuzwe kwenye chama. Ni marehemu Edward Moringe Sokoine ndiye alimwombea msamaha kwa Mwl. Nyerere abadilishiwe adhabu.

Edward Lowasa alipewa adhabu mbadala; kuhudhuria kazini Ofisi Ndogo ya Chama Mtaa wa Lumumba kila siku bila kukosa, kuwa kazini masaa 8 bila kutoka lakini bila kupangiwa kazi yoyote hadi Chama kingeona ametubu na hatimaye apangiwe kazi nuingine. Lowasa alitumikia adhabu yake hadi Sokoine alipofariki.

Hiyo ndio sababu kuu ya Mwl. Nyerere kumkatalia Lowasa kugombea urais.

Kikwete, Mkuchika, Twaha Khalifan, Kinana, Bagenda na Msekwa wanajua ukweli wote kuhusiana na jambo hili. Ila maadamu kwa sasa hakuna tena maadili ya uongozi wa kisiasa nchini Tanzania, Lowassa anaweza kuachiwa awatawale wezi, wala rushwa na mediocre wa nchi hii.

“Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao.”