Yericko Nyerere: Waliokwaza na matokeo ya Udiwani kwa CHADEMA

NINAWASHANGAA WALIOKWAZWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDIWANI HUU KWA CHADEMA

Nimeshiriki hatua zote za uchaguzi katika katika kata 27 nchini, nasema nimeshiriki kwa 100%, sijasimuliwa, wala kusikia tu.

Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi.

Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu nyingi zikiwemo zile zilizozoeleka nyakati zote za uchaguzi kama, kutumia vyombo vya dola, na serikali kwa ujumla kuwadaidia wao.

Hoja ya msingi hapa ni je haya yametokea katika uchaguzi huu tu ama yalikuwepo katika
chaguzi zote?

Kuna wanaoamini kuwa CHADEMA kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "mgogoro" uliochangia kwa 100% kushindwa uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo akini niwape shule ya falsafa ya siasa kidemorasia.

Niwakumbushe kuwa, mwaka 1958 chama cha TANU kikiwa kwenye vuguvugu kali la kupigania Uhuru, kiliwafukuza kabisa uanachama Katibu Mkuu wake Mr Mtevu, na Mwenyrkiti wa Baraza la Wazee ndugu Suleiman bin Amir aliyekuwa na nguvu ya ushawishi hasaaa, walifukizwa waliposhindwa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa shule ya wavulana ya Tabora pale kanda ya Magharibi Tabora na Julius Nyerere akawa rais wa TANU, baada ya uchaguzi ule wao walianzisha uasi kwakuanzisha chama ndani ya chama, chama hicho kilikuwa cha kidini. TANU iliyumba kwa mwaka kamamoja hivi lakini mwaka 1961 ikaingia katika uchaguzi na kushinda.

Kwanza niwaambie kuwa chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapotokea kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo MwanaCHADEMA yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kushindwa uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi mkuu ujao, kwa sasa yanayotokea nikuwa yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa CHADEMA ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo.

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba CCM, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya, idadi kubwa ya wapiga kura hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali kama kuuza shahada zao.

Wanamikakati tukae chini tuwafanyie utafiti wa kisayanzi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao Kikatiba.

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya.

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu.

Yote kwa yote CHADEMA haijapoteza uchaguzi huu, kimkakati ni CCM ndiyo imepoteza.