Agizo muhimu kwa wazazi, walezi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Zanzibar kuhusu sherehe za Eid ul Fitr

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkadam Khamis


Kwa mnasaba wa sherehe za eidul fitr, jeshi la polisi linatoa mwongozo kwa wenye familia na kwa wale wanaotarajia kutembea na watoto wao siku za sikukuu, wawaandikie watoto wao namba za simu za wazazi/walezi na kuzihifadhi katika mifuko ya mashati au suruali au sehemu nyengine yoyote ili iwarahisishie kazi jeshi la Polisi kuweza kujua mtoto na mzazi/mlezi wake na kuweza kuharakisha mawasiliano kwa haraka