[update] Gari lenye viungo vya miili ya wanadamu lakamatwa Dar es Salaam

[update 2] Taarifa kwenye gazeti la MTANZANIA

----

[updae 1] Maoni yangu binafsi yatokanayo na nilichokisikia

Baadhi ya watu walioona viungo hivi vya binadamu wanasema inaonekana vimekaushwa.

Kwa waliopita katika vyuo vya afya, katika somo la elimu ya mwili wa binadamu watafahamu fika kuwa huenda miili hii ni ile inayotumika kwa mafunzo hayo, hasa kutokana na mazingira miili hiyo ilimokutwa kama vile (1) kuwepo kwa wingi wa mipira ya mikononi (gloves), na kama ndivyo, nashawishika kuamini kuwa hizi gloves zilivaliwa na wanafunzi waliokuwa wanatumia ku-dissect cadaver, (2) eneo ni karibu na chuo kimoja cha mafunzo ya wataalamu wa afya na (3) huenda kukauka kulikoelezwa na walioona viungo hivyo ni kwa sababu ya matumizi ya dawa ya kuzuia miili isiharibike (formaldehyde kemikali nyinginezo wanazojua Wakemia) ili itumike kwa mafunzo.

Ikiwa haya ni ya kweli kama inavyoelezwa, basi kwa maana hiyo, ingekuwa vyema kwa Serikali kuhakikisha inalichimbua suala hili ili kufahamu pamoja na mengine:

  • Je, kutupwa kwa miili hii (disposal ya cadaver) kwa aina hii imefanywa katika maeneo gani na kwa muda gani? Hii ni muhimu ili kufuatilia na kuondoa miili na mabaki ya kemikali na madawa hayo kutoka ardhini ambako inaweza kutiririka na kuathiri afya za watu ikiwa dawa hizo zitaingia (penetrate) kwenye mimea hasa ya mbogamboga ambayo hutumika kwa chakula cha binadamu. Tunafahamu fika kuwa kina cha maji (water table) kwa jiji la Dar es Salama kipo juu, hasa nyakati za mvua hivyo ni rahisi sana kwa madawa hayo kutiririka kutoka eneo moja hadi jingine. Vile vile kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa ya ngozi na mfumo wa chakula kutokana na wao kupenda kucheza kila mahala hata kwenye majalala au maji ya mvua yaliyotuama au yaliyoko kwenye mwendo.
Kwa vyovyote vile iwavyo (ndivyo ama sivyo ilivyoelezwa hapo juu) bado kuna uwajibikaji, ambapo pamoja na mengine:
  • Je, ni adhabu gani inayopaswa kutolewa kwa wahusika ili kuzuia jambo hili lisijirudie tena? Wataalamu wa mazingira, wataalamu wa afya na viongozi wa Serikali za mitaa na maeneo husika, hili nadhani ni jukumu linalowahusu moja kwa moja. Ikiwa tunajali afya zetu na uhai wa taifa hili, suala hili lisiingie kwenye mikono ya rushwa kwa maana madhara ya rushwa yatatuathiri sote, rushwa huliangamiza taifa, msituangamize zaidi.Gari lililokamatwa na mifuko yenye viungo ya miili ya wanadamu
Taarifa kupitia blogu ya "Dar es Salaam Yetu" zinasema kuwa Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, limefanikiwa kukamata viungo vya binadamu vikiwa kwenye mifuko ya plastiki katika maeneo ya Bunju/Mbweni Mpiji, Magohe katika eneo ambalo ni marufu kwa uchimbaji wa kokoto nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Viungo vilivyotambulika ni pamoja na miguu na mafuvu ya vichwa vya binadamu.

Jeshi la polisi lipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi.