THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti la Mawio la leo,Alhamisi, Julai 17, 2014, limeandika kwenye ukurasa wake wa kwanza habari yenye kichwa cha habari: “JK, Ukawa wateta”.
Imedaiwa katika habari hiyo kuwa mkutano huo kati ya Rais na ujumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam, wiki iliyopita usiku, kutokana na ombi la Rais.
Habari hizi siyo za kweli. Rais Kikwete hajapata kukutana na kufanya majadiliano na ujumbe wa UKAWA kuhusu mchakato wa Katiba Mpya iwe ndani ama nje ya Ikulu, iwe usiku ama mchana, iwe ndani ama nje ya nchi. Na kwa sababu hajapata kukutana nao ni dhahiri pia kuwa hajapata kuwaomba wakutane naye.
Hata hivyo, Mheshimiwa Rais anaendelea kuamini kwamba ni muhimu kwa UKAWA kurejea Bungeni ili kukamilisha kazi ya kuunda Katiba Mpya inayosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote. Aidha, Rais anaunga mkono jitihada zinazofanywa na watu mbali ili hatimaye UKAWA warudi Bungeni.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Julai,2014