THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Mheshimiwa Jaji Shabani Ally LILA (53) kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 21 Julai, 2014.
Jaji Kiongozi Mteule, Mhe. Jaji Shabani Ally LILA, anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Fakih A.R. Jundu ambaye anastaafu kwa mujibu wa Sherialeo tarehe 20 Julai, 2014.
Jaji Kiongozi Mteule ana uzoefu wa miaka ishirini na miwili (22) katika Mahakama ya Tanzania. Amefanya kazi kwenye Mahakama kama ifuatavyo:-
1992 – 1995- Hakimu Mkazi, Tanga
1995 – 1998- Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lindi
1998 – 2000- Hakimu Mkazi na Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda Ya Songea.
2000 – 2002- Hakimu Mkazi, Mkoa wa Lindi
2002 – 2003- Hakimu Mkazi na Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda Ya Mbeya.
2003 – 2005- Hakimu Mkazi na Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda Ya Dar es Salaam.
2005 – 2006- Hakimu Mkazi, na Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda Ya Arusha.
2006 – 2008- Jaji wa Mahakama Kuu,Kanda ya Dodoma
2008 – 2013- Jaji wa Mahakama Kuu, na Jaji Mfawidhi, Kanda ya Mtwara
2013 – 2014-Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu, akishughulikia uanzishwaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Ilala.
Mheshimiwa Jaji Shabani Ally LILA ana Shahada ya Sheria (LLB Hons) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikohitimu mwaka 1991 na tangu wakati huo amehudhuria kozi fupi, mikutano, semina na makongamano mengi kwenye eneo lake la kazi. Ni mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Majaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma za Jamii (Wafungwa).
Katika kumteua Mhe. Jaji Shabani Ally LILA kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Rais ameridhika kuwa ni mweledi, mchapa kazi, mzalendo, muadilifu na kwamba atakuwa msimamizi na kiongozi imara wa Mahakama Kuu na Mahakama za chini na anamtakia kazi njema.
Aidha, Mheshimiwa Rais, anamshukuru sana Mheshimiwa Jaji Kiongozi Mstaafu,Mhe. Fakih A.R. JUNDU kwa utumishi wake mzuri na mrefu katika Mahakama kwa ujumla na kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano alichokuwa Jaji Kiongozi na anamtakia kila la kheri katika shughuli zake nyingine.
Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
IKULU - DAR ES SALAAM.
20 Julai, 2014