'Diwani ya Kisima Cha Mashairi' ni mkusanyiko wa Mashairi ya Kiswahili yaliyoandikwa na washairi toka East Afrika.Kimajeaa Mashairi ya kisiasa, uchumi, mila na destuli, Mapenzi, Uchumi n.k..
Kitabu hiki ni sehemu ya kwanza ya mkusanyiko wa mashairi yenye dhima na maudhui mbalimbali kutoka katika Kisima cha Mashairi ( https://www.facebook.com/groups/Kisimamashairi).
Kisima cha Mashairi ni kundi la facebook ambalo lengo lake kuu ni kukuza vipaji vya watunzi chipukizi wa mashairi. Kundi hili limeanzishwa Januari mwaka 2013 ikiwa ni wazo la ndugu Msafiri Zombe, Jacob Chenga, Dk. Ally Mvita na Dk.K ahabi Isangula. Katika diwani hii (juzuu la Kwanza), tunawatambulisha malenga chipukizi katika fani hii ya ushairi ambao mashairi yao yametokea kupendwa sana.
Unaruhusiwa kutoa nakala au kusambaza kwa malengo yasiyo ya kibiashara tu na si vinginevyo.