Hoyce Temu |
Pichani ni Mtangazaji anayeongoza Kipindi cha 'Mimi na Tanzania' Hoyce Temu aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 akiwa nje ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili ambapo alimua kufunga safari kwa ajili ya kufanya mazungumzo maalum na Balozi wetu wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula.
Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula katika mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Mimi Na Tanzania, Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC, Marekani. |
Mahojiano hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.
Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema ...Naipenda Tanzania yangu!
Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang'anyi na Balozi Ombeni Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na Balozi wa sasa Mh. Liberata Mulamula.
Hoyce Temu akipiga picha na mmoja wa waliofika Ubalozini kuomba Visa. |
Hoyce Temu akipata picha ya ukumbusho na mpiga picha Iska JoJo aliyerekodi kipindi hicho.
Hoyce Temu anatoa shukrani za pekee kwa blogger "Mzee wa VIJIMAMBO" DJ Luke Joe kufanikisha mahojiano ya Hoyce Temu na Balozi Liberata Mulamula.