Kishindo cha Balozi na Mfalme wa Reggae Jhikoman katika 5th International African Festival Tubingen, UjerumaniNa mdau "Msema Kweli", Tubingen, Ujerumani -- Mfalme wa muziki wa reggae barani Afrika Jhikoman alifanikiwa kufunika kwa kishindo kikubwa katika maonesho ya 5th International African festival Tubingen, siku ya Jumapili, 20 Julai 2014 mjini Tubingen, Ujerumani.

Katika maonesho hayo mwanamuziki Jhikoman kwa sasa ndiye nyota inayong'aa kutoka Afrika katika
muziki wa reggae aliudhihirishia Ulimwengu kuwa Tanzania ni moto wa kuotea mbali kimuziki.

Akishagiliwa na umati wa maelefu ya washabiki waliofika katika maonyesho, Jhikoman anatajwa kuwa ndiye mfalme na nyota mpya ya muziki wa reggae kutoka Afrika.

Jhikoman mwenye maskani yake Bagamoyo mkoani Pwani, Tanzania amekubalika na kupata mkataba na kutumbuiza katika maonyesho mengi barani Ulaya.

(picha kwa niaba ya Afrika Festival Tubingen)