Kuhusu taarifa kuwa Naura Springs hotel imeungua moto

Meneja wa hoteli hiyo, Bi. Beatrice Dallaris akizungumza na wanahabari juu ya taarifa za uzushi zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa hoteli hio imeungua moto Juni 18, 2014.

Utawala na Wafanyaazi wa hotali ya Naura Springs imesikitishwa kwa taarifa zilizosabaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kuwa hoteli yetu inawaka moto na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watu wa mkoa wetu, ndugu na jamaa wa Wafanyakazi wa hoteli, viongozi mbalimbali, vyombo vya usalama, idara ya Zima Moto, waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari na pia kusababisha wasiwasi na kutowesha utulivu na amani wa mji wetu.

Tumesikitishwa sana na tumeomba uongozi wa mkoa wetu walishughulikie swala hili kikamilifu kwani hili sio la kuchukulia mzaha na tungeomba hatua kali zichukuliwe kwa haraka sana kwa alietoa taarifa hiyo ya uongo.

Tunawashukuru watu wote waliofuatilia swala hili na pia tunatoa tamkoa kuwa habari hizi za kuwa hoteli yetu inaungua ni za uongo.

BEATRICE DIMITRIS DALLARIS
HOTEL MANAGER

Sehemu ya jengo la hoteli ya Naura Springs
Picha bandia (ya kutengeneza) iliyosambazwa