![]() |
Washabiki wa Ngoma Africa Band wakipata burudani mjini Tubingen |
Nyuma ya Polisi! Jukwaani FFU! Mbele ya jukwaa washabiki...!
Tubingen,Ujerumani --- Ilikuwa usiku Jumamosi 19, Julai 2014 bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ilipofanikiwa tena kuwatingisha tena malefu ya washabiki katika maonyesho makubwa ya International African Festival 2014 mjini Tubingen, Ujerumani.
Maelfu ya washabiki walijirusha bila ya mashaka na muziki wa FFU-Ughaibuni aka viumbe wa ajabu Anunnaki Alien chini ya uongozi wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja.
Wadau mbalimbali waliohojiwa katika maonesho hayo wameitaja bendi hiyo kila kukicha inazidi kujizolea wingi la umati wa washabiki. Ngoma Africa band inatajwa ndio bendi pekee ughaibuni inayoongoza kuwa na washabiki wa rika, jinsia na mataifa mbalimbali.