Lori ladaiwa kusababsha vifo 17 vya abiria wa basi la Moro Best

Basi la Morobest lenye na namba za usajili T 258 AHV lilipopata jali ya kugongana uso kwa uso na lori na kuua watu 17 katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Basi hilo lilikuwa likitoka Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam

Lori lenye namba za usajili T 820 CKU na tela yenye namba za usajili T390 CKT liliokuwa likiendeshwa na Dereva wake Gilbart Lemanya na utingo wake Mikidadi Zubery Omary ambao wote walifariki papo hapo linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Morobest katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma

Watu zaidi ya 17 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Moro Best wamepoteza uhai baada ya basi hilo kupata ajali mbaya katika eneo la Pandambili katikati ya Dodoma na Morogoro.

Mmoja kati ya mashuhuda wa ajali hiyo Joseph Mtweve aliiambia matukioco.tz kuwa tukio limetokea eneo hilo wakati lori lililokuwa limebeba mabomba kutoka Morogoro kwenda Dodoma likijaribu
kulipita gari jingine mbele eneo ambalo lina kona na hivyo kugongana na basi hilo uso kwa uso.

Alisema watu zaidi ya 12 walikufa papo hapo na wengine watano wanasadikika kufia njiani wakati wakikimbizwa Hospitali kwa matibabu zaidi.

Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo inadaiwa pamoja na dereva wa basi hilo na dereva pamoja na utingo wa lori husika.
Basi la Morobest lenye na namba za usajili T 258 AHV lilipopata jali ya kugongana uso kwa uso na lori na kuua watu 17 katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Basi hilo lilikuwa likitoka Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi kufuatia ajali iliyotokea tarehe 30 Julai, 2014 katika eneo la Pandambili, Wilayani Kongwa na kuua watu wapatao 18.

Katika ajali hiyo, watu 13 walifariki katika eneo la ajali, na majeruhi wapatao 56 walifikishwa hospitalini. Kati ya majeruhi hao hadi sasa waliolazwa ni 30 na wengine wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.

Rais amemuomba Dkt. Nchimbi kumfikishia rambirambi zake za dhati kwa ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, na kuwapa pole majeruhi wote na kuwatakia kupona haraka ili warejee kwenye shughuli zao za kila siku.

“Natoa Pole za dhati kwa wale wote walioondokewa na wapendwa wao katika ajali hii na pia kuchukua nafasi hii kuwapa pole majeruhi wote na kuwaombea kupona haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku”. Rais amesema katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

“Hakika ni jambo la kusikitisha sana kuondokewa na wananchi wetu katika ajali , natoa wito wangu kwa madereva wote na wote wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini wanapokuwa barabarani “. Rais amesema na kuongeza kuwa;

“Kila dereva anaetumia chombo cha moto, ana wajibu wa kulinda maisha yake na ya watumiaji wengine kwa kuwa makini na muangalifu awapo barabarani, kwani ajali hizi zinarudisha nyuma maendeleo ya taifa na ya wananchi kwa ujumla” Rais amesema na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama barabarani kutolegeza kamba katika kuwachukulia hatua madereva wasio makini na wazembe wakati wote”. Rais amesisitiza.

Taarifa kutoka Mkoani Dodoma zinasema ajali hiyo ya jana (30 Julai, 2014) ilisababishwa na Lori ambalo lilitaka kupita lori jingine na hivyo kwenda kugongana uso kwa uso na Basi la Moro Best lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.

30 Julai, 2014

----------

TAARIFA YA POLISI KUHUSU AJALI YA LORI NA BASI LA MORO BEST

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya Dodoma imeongezeka baada ya mtu mwingine kufa .
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime amesema tukio hilo la Pandambili Wilayani Kongwa katika barabara ya Dodoma – Morogoro limesababisha vifo vya watu 18 wanaume watu wazima 11 na mtoto mmoja wa kiume na Wanawake watu wazima 5 na mtoto 1 wa kike.

Majina ya Marehemu hao ambao wametambuliwa na ndugu zao na kusafirishwa kwenda makwao kwa maziko ni:-

1. Christina d/o Dickson, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Mpwapwa
2. Omari s/o Mkubwa, Miaka 32, Muhaya, Kondakta wa bus, Mkazi wa Morogoro
3. Malick s/o Masawe, Miaka 42, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mpwapwa
4. Wilson s/o Paul @ Suda, Miaka 63, Mgogo, Mstaafu Red Cross, Mkazi wa Mpwapwa.
5. Said s/o Lusogo, Miaka 44, mluguru, dereva wa bus, Mkazi wa Kihonda Morogoro.
6. Gabriel s/o Meja @ Chiwipe, Miaka 50, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
7. Gilbert s/o Lemanya, Miaka 53, Mgogo, dereva wa Lori, Mkazi wa Makole Dodoma
8. Mikidadi s/o Zuberi @ Omari Miaka 22, Mbondei, Tingo wa Lori, Mkazi wa Morogoro/Ilala Dar es Salaam.
9. Justine s/o Makasi, Miaka 24, Mgogo, Mkulima wa Mpwapwa
10. Alice d/o Masingisa, Miaka 24, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
11. Merina d/o Doto @ Marcel, Mgogo, Miaka wa Mji mpya Mpwapwa
12. Nasibu s/oSeif, Miaka 48, Mkazi wa Morogoro
13. Nicholaus s/o Raymond Kileo Miaka 51, Mkazi wa Mpwapwa
14. Stella d/o Mdako, Miaka 60, Mkazi wa Mpwapwa
15. Erick s/o Lucas,Miaka 10, Mkazi wa Morogoro
16. Nazaret s/o Deremsi @ Kasuga, Miaka 45, Mhehe, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kibakwe Mpwapwa.
17. DArini d/o Dickson, Miaka 2, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
18. Magreth d/o Nyanzi, Miaka 35, Mgogo, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mwananyamala Dar es Salaam.

Aidha majeruhi waliokuwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa wametibiwa na kuruhusiwa na wengine kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.

Waliobaki katika Hospitali ya Mkoa wakiendelea na matibabu ni 32 na wanaendelea vizuri isipokuwa walio katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu wa madaktari (ICU) ambao ni George s/o Mjelwa, Miaka 40, Daktari wa Wilaya ya Mpwapwa na mke wake aitwaye Getrudar s/o Kombe, Miaka 37, Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

Jana kamanda alisema ajali hiyo baada ya uchunguzi zaidi inaonyesha kusababishwa na madereva wote wawili kwa maana ya dereva aliyekuwa anaendesha lori namba T 820 CKU/T390 CKT GILBERT S/O LEMANYA kwa kupita gari lingine bila kuwa mwangalifu na magari yaliyokuwa yanatokea mbele yake na kuwa katika mwendo kasi.

Dereva wa bus namba T 858 AUH SAID S/O LUSOGO kulingana na mashuhuda hasa abiria wanaeleza alikuwa mwendo kasi na ndiyo maana ajali hii imeleta madhara makubwa kiasi hicho kwani kama angelikuwa kwenye mwendo wa kawaida unaotakiwa madhara yangekuwa siyo makubwa kiasi hicho pamoja na dereva wa lori kufanya aliyofanya.

Wito kwa madereva na watumia barabara wengine waache mwendo kasi na ushabiki wa ushindani kwani kulingana na ushahidi uliokusanywa unaonyesha dereva wa Moro best alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi kutaka kwenda kulipita bus la AL-SAEDY lililokuwa limeondoka mbele yake kwa kigezo kuwa dereva wa bus hilo ni mwanafunzi wake hivyo hawezi kufika Morogoro kabla yake.

Wamiliki wa Ma bus na magari mengine wawaonye madereva wao kuhusiana na mwendo kasi na kuwataka wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali mbaya kama hii.

Aidha abiria wasiwe wanakaa kimya kama walivyofanya wa bus la Moro best wanapoona dereva anaendesha kwa mwendao wa kasi watoe taarifa Polisi ili wakamatwe na kuepusha madhara kama yaliyotokea.

Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.