- Kuitoa wakati wa Sala ya Idd, siku ya Idd yenyewe
- Kuisafirisha kuipeleka sehemu nyengine bila ya dharura
Zakaatul Fitr ni kutumika sehemu inayotolewa kama kuna wanaostahiki na wanahitaji. Kama hakuna hapo inajuzu kuisafirisha kuipeleka sehemu nyingine na huwajibika kwa mwenye kuitoa kwa njia hii kuhakikisha kwamba aliowapa ni watu thika wanaoaminika na ni kweli wataifikisha kwa wahusika kabla ya siku ya Idd. Vyenginevyo bado mtoaji atakuwa na dhimma kwa Zakaah hii ikiwa haikuwafika walengwa katika muda unaotakiwa
- Kutoitoa kabisa
- Kuchanganya kati ya Zakaatul Fitr na Zakaatul Maal
Na wanaowajibika kuitoa wana hukumu tofauti na Zakaah ya mali. Hivyo lazima itolewe bila ya kuihusisha na Zakaah ya mali.
- Kuitoa na kuwapa pesa wanaostahiki badala ya chakula
- Kuwapa Zakaatul Fitr wasiokuwa Waislamu
- Zakaatul Fitr kutumika katika miradi mengine
Zakaatul Fitr haiwezi kutumika katika malengo yasiyokusudiwa hata kama yatakuwa ni ya kheri kwani dini yetu ina taratibu zake kwa kila kinachotolewa kwa mujibu wa munasaba wake. Zakaah hii ni kwa ajili ya wanaohitajia miongoni mwa Waislamu na si vyenginevya na kiwango chake ni kidogo mno ambapo kila mmoja wetu ana uwezo wa kukitoa.
Na Allaah ndie ajuaye.