Marekani yasitisha shughuli zote za US Peace Corps nchini Kenya

BBC inaarifu kuwa Shirika la Marekani la kutoa misaada ya matibabu US Peace Corps limetangaza kuwa linasitisha shughuli zake zote nchini Kenya na taryari limeamuru kuondolewa kwa wafanyikazi wake wote zaidi ya hamsini kutoka nchini humo.

Marekani majuzi ilikuwa imetangaza kupunguzwa kwa idadi ya wafanyikazi katika balozi yake iliyoko mjini Nairobi.

Aidha ripoti hiyo inawadia siku mbili baada ya Shirika linalosimamia usafiri wa Anga ya Marekani kupiga marufuku safari zote za ndege katika anga ya Kenya.

Hatua ya shirika la US Peace Corps kuwaondoa wafanyikazi wake kutoka Kenya imechukuliwa muda mfupi baada ya wanawake watatu kutiwa nguvuni nchini Marekani (katika jimbo la Virginia na mwingine Washington) na Uholanzi kwa madai ya kutoa ufadhili kwa kundi la wanamgambo wa kiislam wa al-Shabab nchini Somalia.

Washukiwa hao wanadaiwa kutuma pesa katika mtandao wa malipo madogo madogo kila mwezi.

Wizara ya sheria ya Marekani imesema kuwa washukiwa wengine wawili akiwemo Jama Mohammed Fardowsa wamejificha nchini Kenya na Somalia.