Meya wa Ilala akagua ukarabati wa barabara Ukonga Mazizini - Moshi Bar

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara (mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano (katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Ukonga-Mazizini mpaka Moshi Bar.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Ukonga - Moshi Bar ya urefu wa kilometa tatu kwa kiwango cha changarawe awamu ya kwanza, ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa
miundo mbinu uliotokea baada ya mvua kubwa.

Mradi huo ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90, pesa za ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Barabara hiyo itawekwa lami ndani ya mwaka huu.



Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.




Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.




Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.




Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar




Mwonekano wa Bara barabara hiyo




Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.




Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.




Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo




Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.

Tumeshirikishwa taarif hii na Dj Sek Blog