Moto mkali wa Jhikoman kutoka Bagamoyo hadi Ujerumanni


Tubingen, Ujerumani -- Mwanamuziki maarufu wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania, alifanikiwa kuwadatisha akili washabiki wa muziki nchini Ujerumani siku ya Alhamisi, 17 Julai 2014 katika maonesho makubwa ya kimataifa ya 5th International African Festival Tubingen 2014, yanayofanyika katika viwanja vya Festplatz, mjini Tubingen, Ujerumani.

Mwanamuziki huyo nguli wa reggae amepewa heshima zote za Kimataifa kwa uwakilishaji wake kama balozi wa reggae wa Afrika.

Ratiba ya maonesho hayo inaonyesha kuwa Jhikoman atapanda tena jukwaani siku ya Jumapili, 20 Julai 2014 jioni kutokana na maombi maalumu ya washabiki waliotaka kumuona tena mflame huyo wa reggae.

Pia taarifa zimetosa kuwa Jumamosi 19 julai 2014 saa 2.00 usiku FFU-Ughaibuni aka Ngoma Africa band watatumbuiza katika maonyesho hayo.

www.jhikoman.com