Moto waunguza nyumba ya Rais wa TFF, Malinzi

Na CLEZENCIA TRYPHONE -- RAIS wa Shirikishola Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinzi, ameunguliwa na nyumba yake, mjini Bukoba jioni ya leo.

Akizungumza na Habari Mseto Blog leo, Malinzi amesema, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, ambapo kila kitu kilichokuwemo ndani ya nyumba hiyo kimeteketea.

Amesema, licha ya mali zote kuteketea hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto, ambapo kesho anatarajia kwenda kuangalia athari zilizotokana na moto huo.
"Nimeunguliwa na nyumba yangu, iko Bukoba, lakini namshukuru mungu hakuna aliyejeruhiwa, kesho naondoka kwenda Bukoba," 
amesema Malinzi na kuongeza kuwa, hakuna kitu chochote kilichookolewa katika ajali hiyo.

---
Imenukuliwa na wavuti.com kutoka Habari Mseto blog