JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI

Telegrams TEMESA DSM S.L.P 70704
Simu: +255-22-2862796/97 DAR ES SALAAM
Fax: +255-22-2865835 TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) anawatangazia wananchi wote kuwa kivuko cha MV. Kigamboni kinatarajiwa kwenda kwenye matengenezo makubwa wakati wowote kuanzia leo.
Hivyo huduma za uvushaji zitaendelea kwa kutumia vivuko vya MV. Magogoni pamoja na MV. Lami katika kipindi chote cha matengenezo husika.
Uongozi wa TEMESA unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu
TEMESA
23/7/2014