Nipashe, The Guardian yashirikiana na Vodacom kutoa taarifa "Breaking News" kwa njia ya simu ya mkononi

Meneja Masoko wa kampuni ya The Guardian na Nipashe, Simon Marwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa huduma mpya itakayokuwa inatumiwa na wateja wanaotumia mtandao wa simu za mkononi wa vodacom kupata habari za punde (Breaking News)za kitaifa na kimataifa kupitia magazeti ya Nipashe na The Guardian, mahali popote na muda wowote. Ili kujiunga mteja anatakiawa kuandika neno Nipashe au The Guardian kwenda namba 15501. Kushoto ni Meneja Uendeshaji Premier Mobile Solution Lulu Ramole na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa.

Dar es Salaam, 24th July 2014 - Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na The Guardian Limited wachapishaji wa magazeti ya The Guardian na Nipashe imezindua huduma mpya ya kufikisha habari za punde (Breaking News) kwa jamii, kuanzia leo.

Ujio wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azima ya makampuni yote mawili ya kutaka kuona wananchi wakiwa na njia bora na ya uhakika ya kupata taarifa mbalimbali mara tu zinapotokea.

Huduma hii mpya itakayojulikana Kama‘GUARDIAN SMS na NIPASHE SMS ni huduma iliyobuniwa kuhakikisha mamilioni ya watanzania wanaotumia mtandao mkubwa wa kampuni ya Vodacom wanapata habari kwa haraka na za motomoto kupitia simu zao za kiganjani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa amesema kuwa Vodacom inafurahi kuungana na magazeti ya The Guardian na Nipashe kuanzisha huduma hiyo chini ya kampuni ya Premier Mobile Solution.

Twissa amesema huduma hiyo itakayo wahusisha wateja wa Vodacom itasaidia kuwawezesha wateja hao kupokea taarifa mbalimbali kupitia simu zao za mkononi kwa gharama nafuu ya Sh 100 kwa siku.

“Mteja wa Vodacom ataunganishwa na huduma hii kwa kupeleka ujumbe wenye neno GUARDIAN au NIPASHE kwenda namba 15501, kwa gharama nafuu kabisa ya Sh100 kwa siku, na baada ya hapo atakuwa akipokea taarifa mbalimbali kutoka vyumba vya habari vya magazeti ya The Guradian na Nipashe”

Naye Meneja Masoko wa kampuni ya The Guardian Simon Marwa ameitaja huduma hiyo kuwa itawawezesha wasomaji wa magazeti ya hayo ambao ni wateja wa mtandao unaoongoza nchini wa Vodacom kupata habari za punde kirahisi.

“Huduma hii ni muhimu kwetu na kwa vodacom kwani wasomaji wa magazeti haya sasa watakuwa na uwezo wa kupata habari za punde za kitaifa na kimataifa kiurahisi kupitia simu za viganjani.”Alisema Marwa

“Vodacom imeenea nchi nzima hivyo ubunifu huu wa upashanaji habari wananchi wa njia ya kisasa ni wazi utawanufaisha walio wengi na kutaleta utofauti kwa jamii.”Alisema Marwa.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Premier Mobile Solution Lulu Ramole amesema huduma ya Nipashe SMS na The Guardia SMS imebuniwa wakati muafaka ambapo jamii ina mwamko wa kupata taarifa mbalimbali.

“Ni furaha kubwa kwetu kuona tunasimamia huduma inayowaleta pamoja makampuni mawili makubwa katika nyaja ya Mawasiliano na Habari.Tumejipanga kuiwezesha huduma hii kuwa bora zaidi”Alisema Lulu

Ameongeza kuwa mteja ana uhuru wa kujiunga na kujiondoa wakati wote atakapojisikia kufanya hivyo kwa kutuma neno STOP au ONDOA kwenda namba 15501 kutoka simu yake ya mkononi.

Aliongeza kwamba huduma hii itatolewa kwa saa 24.