PPF na MSD wasaini mkataba wa “wekeza”; Wafanyakazi 400 wa MSD wajiunga PPF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, wakiweka saini mkataba wa “Wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014. Chini ya Mkataba huo, zaidi wa wafanyakazi 400 wa MSD wamejiunga na PPF. 
Viongozi wa PPF na wenzao wa MSD, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa MSD waliokabidhiwa kadi za uanachama wa Mfuko huo, mara baada ya kutiliana saini mkataba ambapo MSD na PPF zimekubaliana kuanzisha mpango wa "Wekeza" ambapo wafanyakazi wa MSD sasa watakuwa wakichangia kwenye mfuko huo ili kujiwekea akiba na kujipatia mafao mbalimbali.