![]() |
Balozi Seif akibadilishana mawazo na mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete huk Wete, Pemba. |
Na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ - Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu nchini kuendelea kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao kama inavyoagiza wakati wote.
Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili ya Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya Ikulu ya Serikali ya Muungano yaliyopo Mjini Wete Pemba.
Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa Waislam hupatikana katika mjumuisho wa
makundi ya ibada akiyataja kuwa ni pamoja na madrsasa, sala pamoja na mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futari ya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao.
Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa Zanzibar.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada hiyo.
Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia hufanywa ba baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni katika kujipatia futari.
![]() |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa shukrani kwa niaba ya Rais Kikwete mara baada ya futari ya pamoja kwa wananchi wa mikoa miwili ya Pemba |
![]() |
Balozi Seif akiwaaga na baadhi ya wananchi wa mikoa miwili ya pemba waliohudhuria futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete hapo Ikulu ya Wete, Pemba. |