Rais Obama leo kukutana na Viongozi Wadogo walioonesha dira toka nchi zote za Afrika

Joshua Nassari, Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA)

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiingia kwenye ukumbi wa mkutano ambao baadaye yeye na viongozi vijana wenzie watakutana na Rais Barak Obama wa Marekani atakapozungumza nao jijini Washington DC.

Hii ni sehemu ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote za Afrika (most promising young African leaders). Program hii imeanzishwa na Rais Obama mwenyewe.

Miongoni mwa watanzania wachache waliopata fursa ya kuhudhuria ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Steven Masele na Mhe. Joshua Nassari. Watakutana pia na Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Mke wa Rais Obama Bi Michelle Obama Pamoja na maseneta, Magavana, wafanyabiashara wakubwa an watu wengine mashuhuri.