Mkuu wa shule hiyo, Kevin Mlengule amenukuliwa akisema kuwa pamoja na walimu hao shule iliwafukuza wanafunzi wa kike 2 waliobainika kukubuhu kwa ngono.
Alisema kura ya siri iliyopigwa dhidi yao ndiyo iliyowabaini walimu na wanafunzi hao kuwa
wanajihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ya watumishi na wanafunzi.
Alisema kura ya siri iliyopigwa dhidi yao ndiyo iliyowabaini walimu na wanafunzi hao kuwa
wanajihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ya watumishi na wanafunzi.
“Katika kuboresha nidhamu kwa watumishi na wanafunzi wawapo shuleni jambo moja lililokuwa linatusumbua na tukaamua kulitafutia dawa kali ni la mahusiano ya mapenzi kati ya walimu na wanafunzi, na wanafunzi na watu wa mitaani,”
Alisema miaka mitatu iliyopita lilikuwa ni jambo la kawaida kwa wanafunzi wa kike kujihusisha katika mapenzi na walimu wao pamoja na watu wengine kutoka mitaani.
Hali hiyo ilisababish baadhi ya wanafunzi wenye tabia hiyo kufuatwa “na wanaoitwa mabwana zao” shuleni muda wowote na kutoroshwa. Alisema hali hiyo ilichangia kuporomosha taaluma shuleni hapo na kufanya matokeo ya wanafunzi wanaomaliza shule hiyo kuwa mabaya kwa muda mrefu.

Mlengule alisema matokeo hayo yaliwafanya baadhi ya wazazi kuwahamisha watoto wao kutoka katika shule hiyo na kuwapeleka shule nyingine.
“Shule ilikuwa na wastani wa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita 2,500 kila mwaka, matatizo hayo na mengine yaliyokuwepo yaliifanya ibakiwe na wanafunzi wasiozidi 600.”
Alisema katika kukabiliana na utovu wa nidhamu:
“hatuna mzaha hata kidogo, mwalimu na mwanafunzi atakayebainika akijihusisha na ngono katika mazingira yoyote yale wote kwa pamoja tunawafukuza.”
Aliwataka wazazi waliohamisha wazazi wao shuleni hapo kutoihofia tena hali hiyo kwani imedhibitiwa vya kutosha.