Siasa at its best? Hata uichukie siasa, itakuchekesha tu! Waliokuwa Madiwani CHADEMA Shinyanga na kuhamia CCM warejea CHADEMA

"Tunavua uCCM" kama walivyovua magwanda ya CHADEMA mbele ya Nape Nauye wa CCM, leo madiwani hao wamevua pia nguo za CCM, lakini tofauti na kipndi kile leo hawakuchoma moto nguo.

Picha na maelezo kutoka kwa Kadama Malunde wa Malunde1 blog 

Ilikuwa siyo hali ya kawaida - wengi walibaki midomo wazi, walipigwa na hali ya mshangao, wenye kushika viuno haya, wenye kununa haya, wenye kutukana sawa, wenye kusema bora liende nao walikuwepo, wenye kuisikitikia CHADEMA kwa kupokea watu wanafiki na wasaliti twende, wenye kukumbuka mbwembwe za CCM wakati wa kuwanyakua Madiwani hao tena katika eneo hilo nao hawakukosekana....


... pichani ni wananchi wakiwa na Hasira kuona madiwani waliowaita wasaliti wakirudi CHADEMA tena. Hapa ni katika viwaja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo Nane mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa aina yake ambao pengine unaweza kuuita mkutano wa kihistoria, mkutano
ambao uliandaliwa na viongozi wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki wakiongozwa na Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi.

Katika mkutano huo, wale madiwani wa CHADEMA ambao mwezi Februari mwaka huu (bofya hapa kurejea habari hiyo), walijiuzulu na kuhamia CCM, Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo na Sebastian Peter wa Kata ya Ngokolo, leo wameomba radhi na kurudi CHADEMA.

Miongoni mwa sababu walizozitaja kuchangia kuhama kwao CCM ni chama kinachochonganisha vyama walidanganywa kuhamia ACT lakini wamebaini kuwa ACT na CCM hawana tofauti hivyo kuamua kurudi CHADEMA kwani ndiyo chama imara.

Walisema waliahidiwa kuwa wahame CHADEMA waende CCM ili wajiunge na ACT ili waiimarishe lakini wameshindwa kutofautisha CCM na ACT.

Ikumbukwe kuwa walihamia CCM wakidai CHADEMA hakifai kinaendekeza ubinafsi, ukabila n.k, ikafikia hatua wakaitwa madiwani mizigo.

picha ya kumbukumbu ya tukio la mwezi Februari mwaka huu


Aliyevaa nguo ya kijani (CCM) ni bwana Zacharia Mfuko diwani wa CHADEMA kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwasili katika mkutano wa Chadema leo jioni, baadaye alivua nguo hizo na kuomba radhi kuwa alikosea njia baada ya kushawishiwa na viongozi wa CCM akiwemo Stephen Masele, Nape Nauye, Habib Mchange na viongozi wengine wengi ndani na nje ya CHADEMA na CCM, na kueleza kuwa CCM hawana lolote badala ya kulaghai watu.Kulia ni Sebastian Peter diwani wa Ngokolo akiwasili katika eneo la mkutano, leo. Katika hali ya kushangaza baada ya madiwani hao kuwasili kwenye mkutano vurugu za hapa na pale zilitawala takribani dakika 15 lakini baadaye hali ilikuwa shwari baada ya mbunge Kasulumbayi kutumia akili na nguvu nyingi kutuliza wanachama wa CHADEMA waliokuwa na hasira na kutopendezwa na kitendo cha kuwaleta wasaliti wa chama eneo hilo.


Diwani Sebastian Peter kulia akinong'ona jambo na mbunge Kasulumbayi. "Madiwani wasaliti" kama wanavyoitwa hivi sasa hapa Shinyanga, wakiwa na nguo za CCM wakiwa wamekaa na viongozi wa CHADEMA baada ya kuwasili eneo la mkutano jioni ya leo.


Kushoto ni Zacharia Mfuko baada ya kuvua nguo za CCM,akiwaomba msamaha wanachama wa chadema na wananchi kwa ujumla.Alisema walihadaiwa na CCM,kamwe hatarudia kosa na kuongeza kuwa hata nguvu za giza/dawa zilitumika kuwachanganya akili ili waidharau chadema lakini sasa wamegundua ujanja wa ccm na kuwatahadhalisha wengine wenye nia ya kwenda CCM waache kwani halifai.


...Hiki ninachokiona ni ndoto, mazingaombwe au ndiyo kile waungwana wanachosema kuwa siasa ni mchezo mchafu....


Mbunge Kasulumbayi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwakaribisha madiwani hao na kwamba sasa ni madiwani tena kwa sababu wakati wanajiuzulu hawakufuata taratibu kama vile kwenda mahakamani,kwasilisha vitambulisho vya udiwani na vyeti vyao vya ushindi na kuwashangaa CCM kwani hawako makini kwa sababu hawakujua kuwa watu waliowachukua ni wajanja kwa vile hata kadi za ccm hawakuchukua na wamefanikiwa kujua siri za ccm.


Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga bi Siri Yasin akifunga mkutano leo jioni.

Shukurani: Malunde1.blog