Stashahada ya Uuguzi kwa Njia ya Masafa (e-Learning Programme)

Je, wewe ni muuguzi uliyejiandikisha? Unataka kujiendeleza ili uweze kuwa muuguzi aliyesajiliwa?

1.Usuli

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa Tanzania, inawakaribisha waombaji wanaopenda kusomea Diploma ya Uuguzi inayotolewa kwa njia ya masafa au kielektroniki (eLearning). Programu ya kutoa mafunzo kwa masafa ilizinduliwa mwezi Aprili, 2011 na Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Rasilimali Watu kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. Lengo la kozi hii ni kuboresha utoaji wa huduma ya afya kwenye jamii nchini Tanzania. Utoaji wa mafunzo kwa njia ya masafa huwawezesha wakunga kuendelea kuwepo kwenye vituo vyao vya kazi kwa sehemu kubwa ya muda wa mafunzo. Wanafunzi wa awamu ya kwanza ya mpango huu wanatarajia kuhitimu mafunzo yao Aprili 2015.
2.Mtalaa

Programu hii inatumia mtaala wa kitaifa nchini Tanzania ambao unatumiwa na vyuo vya uuguzi vya stashahada.

Kozi itaendeshwa kwenye vyuo saba (7 ) vifuatavyo:
1)Mikocheni School of Nursing, Dar es Salaam

2)Muhimbili School of Nursing, Dar es Salaam

3)Muheza School of Nursing, Tanga

4)College of Health Sciences Zanzibar

5)Shirati School of Nursing, Mara

6)Bugando School of Nursing, Mwanza

7)KCMC School of Nursing, Kilimanjaro

Waombaji wanashauriwa kuomba kwenye vyuo vilivyokaribu nao ili kuepuka gharama kubwa za kusafiri wakati wa mafunzo ya ana kwa ana mwanzoni mwa mihula.
3.Masharti ya kujiunga na kozi


Masharti ya kujiunga na programu ya Stashahada ya Uuguzi kwa njia ya masafa ni sawa na masharti ya kujiunga na kozi nyingine yeyote ya Stashahada ya Uuguzi nchini. Mwombaji anatakiwa kutuma barua ya maombi ambayo imeandikwa kwa mkono ikiambatanishwa na hati zifuatazo:
  • Nakala ya vyeti vya uuguzi na ukunga
  • Nakala ya leseni ya sasa ya kufanya kazi kama muuguzi na mkunga aliyeandikishwa rasmi na Baraza la uuguzi na ukunga Tanzania.
  • Nakala ya vyeti vya elimu ya sekondari (CSEE) vyenye ufaulu wenye walau ‘D’ Nne,’D’ mojawapo sharti iwe ya ama baolojia au kemia.
4.Ada ya mafunzo
a)Wote watakaojiunga na mafunzo haya watatakiwa kulipa adaya Tsh. 100,000/= kwa ajili ya mitihani. Ada ya mitihani inapaswa kulipwa kabla ya kufanya mitihani ya kuhitimu. Utaratibu kamili wa kulipwa utaelezwa na mkuu wa chuo
b)Kwa vyuo vya uuguzi vya binafsi, ada ya mafunzo itaamuliwa na vyuo na kulipwa kwenye Chuo husika.
ØMikocheni – S.L.P 65300 DAR ada sh. 1,025,000/= kwa mwaka
ØShirati – S.L.P 10 Shirati - Rorya ada sh. 500,000/= kwa mwaka, email: [email protected]
Simu: 0763 317 089
Ø Muheza School of Nursing, S.L.P 5 Muheza, simu adani Tshs 740,000/= (laki saba na arobaini elfu )kwa mwaka. Email M[email protected] simu 0685 357 399 Mkurugenzi na [email protected]Mratibu wa mafunzo ya masafa
a) Kwa vyuo vya uuguzi vya serikali vifuatavyo ada ni sh. 365,000/= kwa mwaka na italipwa kwa mkuu wa chuo mara baada ya kuripoti chuoni
ØBugando School of Nursing, S.L.P 476 Mwanza, landline; +255-(0) 28-2540610 ext. 218 or 250,
email [email protected], Fax: +255-(0) -28-2500799
ØKCMC School of Nursing, S.L.P 3012 Moshi, wasiliana kwa simu hii: 0769 747 996
ØMuhimbili – S.L.P 65004 DAR
b)Kwa chuo cha Zanzibar
College of Science, S.L.P 1898, Zanzibar. Webwww.chs.ac.tz fees Tsh. 365,000/=
5.Namna ya kutuma maombi
Fomu za maombi zitapatikana katika vyuo husika vya uuguzi na katika tovuti ya Wizara ya Afya na Amref Health Africa Tanzania
c)Upande wa vyuo vya uuguzi vya serikali, mwombaji atatakiwa kulipia shilingi elfu thelathini (30,000/) ambazo hazitarejeshwa kwa mwombaji. Mwombaji atatakiwa kulipa fedha hiyo katika chuo anachoomba mafunzo hayo, wakati akiwasilisha fomu ya maombi.
d)Kwenye fomu ya maombi ambatanisha:
i.Picha moja ya pasipoti ambayo umepigwa hivi karibuni
ii.Barua kutoka kwa mwajiri inayothibitisha kwamba mwombaji ana uzoefu kazini usiopungua miaka miwili.
e)Waombaji ambao walisomea nje ya Tanzania, watatakiwa waambatanishe hati toka Baraza la Mitihani la Taifa, zenye sifa zinazolingana na sifa zilizo kwenye vyeti vinavyotoka kwenye mamlaka za nchi husika.
f)Baada ya kujaza fomu wasilisha kwenye chuo cha uuguzi husika kabla ya tarehe 20 Septemba , 2014
g)Usaili na uchaguzi utafanyika wiki ya mwanzo ya October 2014. na wote mtataarifiwa siku ya usaili kwa njia ya simu na barua.
h)Tarehe ya kuanza kwa mafunzo itatangazwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa watakaochaguliwa.
i)Muombaji awe amemaliza kozi ya cheti kuanzia mwaka 2012 kurudi nyuma.
6.Terehe ya kuanza na muda wa kozi

Waombaji watakaochaguliwa watajulishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tarehe ya kuripoti vyuoni na ambapo wanapaswa kwenda. Kila mwanzo wa muhula wanafunzi watahudhuria mafunzo ya ana kwa ana; na watapata fursa ya kufanya mazoezi kwa vitendo ili kupima ujuzi wao wa msingi katika mafunzo ya uuguzi. Pia kutakuwa na vipindi vya mafunzo kuhusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Baada ya hapo watapitia mafunzo katika vituo vya mafunzo kwa njia ya masafa vilivyopo kwenye vyuo vya uuguzi husika. Pia, wanafunzi watapewa msaada wa mara kwa mara na usimamizi kutoka kwa wakufunzi na washauri katika hospitali (mentors). Katika programu hii, Amref Health Africa itakuwa inatoa msaada wa kiugavi na kiufundi kwenye mchakato mzima wa mafunzo kwa njia ya masafa.


Kwa maulizo, tafadhali wasiliana na: Amref Health Africa, Tanzania

Barabara ya Ali Hassan Mwinyi; SLP 2773, Dar es Salaam,

Namba za Simu: +255 22 2116610/2131981/2136731/2153104 au +255 716 533115/0757451032 Namba ya Faksi: +255 2115823; Barua Pepe: [email protected]; Tovuti: www.amref.org

AU

Ministry of Health and Social Welfare, Box 9083, Dar es Salaam,

Tel: +255 22 2120261, Fax: 2139951; website: www.moh.go.tz